Pages
▼
Pages
▼
Saturday, June 30, 2012
MISS TOURISM KINONDONI 2012 WATEMBELEA FRIDAY NIGHT LIVE JANA USIKU
Baadhi ya warembo wanaoshiriki Miss Tourism Kinondoni wakiwa ndani ya gari wakielekea katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV.
miss kinondoni anaetarajiwa kukabidhi taji akiwa na wancy model
miss kinondoni anaetarajiwa kukabidhi taji akiwa na wancy model
Friday, June 29, 2012
KUMEKUCHA MISS UTALII KINONDONI 2012
RAY AZINDUA FILAMU YA SOBBING SOUND KWA KUTOA MSAADA AKISHIRIKIANA NA STEPS
Msanii wa filamu nchini Vicent Kigosi 'Ray' akikabizi sehemu ya msaada
uliotolewa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam leo
kwa Mlezi wa kituo cha Maunga Centre kilichopo Kinondoni Zainabu
Bakari vyakula mbalimbali vimetolewa vyenye samani ya shilingi milioni
moja na nusu katika kituo hicho kushoto ni Meneja Masoko wa Kampuni ya
Steps, Ignatus Kambarage.Picha na Mpiga picha Wetu
Msanii wa Filamu Nchini Visent Kigosi 'Ray' katikati na Meneja Masoko wa
Kampuni ya Steps.Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja baada
ya lei kugawa vyakula mbalimbali katika kituo cha kulelea watoto yatima
cha Maunga Centre vilivyotolewa na Kampuni ya Steps wakati wa Uzinduzi
wa filamu yao Mpya ya Sobing Sound.Picha na Mpiga Picha Wetu
ZANZIBAR FILM FESTIVAL July 5
Mwaka huu mastaa kibao watashuka Bongo. Kutoka Marekani anakuja Mario
Van Peebles. Kama umeangalia filamu ya All Things Fall Apart ya 50
Cent utakuwa umewahi kumuona huyu jamaa, mle ndani aliigiza kama baba
wa 50 Cent.
Cabo Snoop naye atadondoka kutoka Angola, yote ni kuzifanya siku tisa
za tamasha zisimchoshe mtu yoyote, bila kwuasahau mastaa wetu Bongo
kama Diamond, Linah, Barnaba, Roma na Sultan King.
Bongo Movies wao ndio wataongoza jahazi la filamu, JB, Davina, Irene
Uwoya, Jackline Wolper, Cloud na wengine wengi wataheadline katika
tamasha.
Van Peebles. Kama umeangalia filamu ya All Things Fall Apart ya 50
Cent utakuwa umewahi kumuona huyu jamaa, mle ndani aliigiza kama baba
wa 50 Cent.
Cabo Snoop naye atadondoka kutoka Angola, yote ni kuzifanya siku tisa
za tamasha zisimchoshe mtu yoyote, bila kwuasahau mastaa wetu Bongo
kama Diamond, Linah, Barnaba, Roma na Sultan King.
Bongo Movies wao ndio wataongoza jahazi la filamu, JB, Davina, Irene
Uwoya, Jackline Wolper, Cloud na wengine wengi wataheadline katika
tamasha.
JB akizungumza katika mkutano na wanahabari, pembeni ni Davina.
Thursday, June 28, 2012
WAREMBO WA MISS UBUNGO
Mashindano
ya Urembo ya Redd’s Miss Tanzania 2012 yanaendelea kwa kasi kubwa na
kwa wiki hii kutakuwa na shindano moja kubwa hapa jijini Dar es salaam
ambapo kituo cha Ubungo yaani “REDD’S MISS UBUNGO 2012” kitakuwa kikifanya shindano lake.
Shindano hili litafanyika Ijumaa hii ya tarehe 29 / 06 / 2012 katika Ukumbi wa Hotel ya LANDMARK iliyopo ubungo kuanzia saa mbili usiku..
kiingilio katika shindano hili kimepangwa kuwa tsh. 10,000/= tu na burudani itakayosindikiza shindano hili itatoka kwa bendio ya FM ACADEMIA (wazee wa ngwasuma)
kituo
hiki cha miss ubungo ndicho kilichomtoa Miss Tanzania 2004 FARAJA
KOTTA, hivyo ni mategemeo yetu tutatoa tena Miss Kinondoni na hatimae
ndie atakaekuwa REDD’S MISS TANZANIA 2012.
Jumla
ya warembo kumi na sita wamejitokeza kuwania taji hili wakiwa chini
ya mwalimu wao BEATRICE JOSEPH ambaye alikuwa Miss Ruvuma 2004 na kwa
upande wa shoo ya ufunguzi wanafundishwa na BOKILO ambaye ni
mwanamuziki kutoka TOT BAND.
Wednesday, June 27, 2012
DKT ULIMBOKA AZUNGUMZA KILICHOMPATA
Mweneyikiti wa Jumuia ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka, amepigwa na kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika.
Dkt
Ulimboka anadaiwa kuvunjwa mbavu, miguu yote miwili, kung’olewa meno
yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio
hilo la kikatili na kusikitisha limetokea usiku wa kuamkia leo jijini
Dar es Salaam, na linadaiwa kufanywa na watu wa sio julikana ambapo
kabla ya kufanya unyama huo walidaiwa kumteka na kumpiga kabla ya
kumtelekeza katika eneo la msitu wa Pande Mabwepande.
DKT. ULIMBOKA ASIMULIA TUKIO
Akisumulia
tukio hilo Dkt Ulimboka alisema kuwa jana usiku alipigiwa simu na mtu
aliyejitambulusha kwake kuwa anaitwa Hemed, aliyemwambia kuwa anahitaji
kuongea naye, na ndipo walipopanga kuonana katika eneo la Leaders
Kinondoni.
Dk
Ulimboka aliyekuwa akiongea kwa tabu, aliendelea kusimulia kuwa wakati
akiongea na mtu huyo anayekiri kuwa alikuwa akifahamiana naye kabla,
alikuwa na wasiwasi kwani kila mara alikuwa akipokea simu na kuwasiliana
na watu wengine ambao hawakuwapo eneo hilo.
Alisema
baada ya muda alishangaa kuona wanaongezeka watu wengine watano wakiwa
na silaha, kisha wakamwambia kuwa anahitajika kituo cha Polisi na
kumvuta na kumuangusha barabarani kabla ya kumuingiza katika gari lenye
rangi nyeusi na kuondoka naye.
Dkt
Ulimboka alisema kuwa wakiwa njiani walimpiga, na kumfikisha katika
msitu huo wa pande na kuendelea kumpiga paka alipoteza fahamu.
MADAKTARI NAO WALONGA
Akisimulia
mkasa huo mmoja wa madaktari wenzie aliyefahamika kwa jina moja la Dkt
Deo, alisema kuwa alipigiwa simu na mtu hasiyemfahamu na kumfahamisha
tukio hilo.
Alisema
alipofika katika kituo cha Polisi cha Bunju, alimkuta akiwa katika hali
mbaya na ilikuwa ngumu kumtambua kwakuwa alikuwa na majeraha mengi eneo
la usoni.
Aliongeza kuwa akiwa na wenzie waliamua kumchukua na kumkimbiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya matibabu.
"Hali
yake kwakweli ni mbaya sana, amepigwa mno na ameumizwa kwakweli
tumemleta hapa hili aweze kupata matibabu, lakini mimi nilivyomkuta mara
ya kwanza nilishindwa hata kumtambua kwa jinsi alivyokuwa
ameumizwa"alisema Dkt Deo
Alisema
kuwa alisimuliwa na Dkt Ulimboka kwamba watu hao waliomteka na kumpiga
walikuwa na silaha na kwamba alishindwa kuwatambua.
Aliongeza
kuwa Dkt Ulimboka alidai kuwa wakati akiwa katika halimbaya alikuwa
akisikia mazungumzo yao, wakibishana juu ya kumuua wengine wakisisitiza
achomwe sindano, na wengine wakitaka kumpiga risasi.
Alisema
wakati mabishano yakiendelea kati yao, Dkt Ulimboka aliinuka akiwa na
lengo la kukimbia lakini watu hao walipiga risasi hewani iliyomshtua na
kuangua chini.
Kwa
upande wake Dkt Cathbeth Mcharo ambaye ndiye aliyempokea Dkt Ulimboka
Hospitalini hapo, alisema kuwa hali yake ni mbaya na kwamba wanajitahidi
kumpatia huduma za haraka.
Alisema kuwa kwa hatua za awali amefanyiwa vipimo mbalimbali, hili iweze kufahamika aina ya matibabu anayotakiwa kupatiwa.
POLISI
Kamanda
wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova
amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na
kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka
anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya
Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda
Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka
kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema
huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa
kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua
maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa
ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda
Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa
ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni
tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote
watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na
sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo
MUHIMBILI
Wakati
hayo yakitokea inadaiwa kuwa Askari Kanzu mmoja alikumbana na kipigo
kikali kutoka kwa madaktari hapo Muhimbili kwa kile kilochodaiwa
kutambuliwa na Dkt Ulimboka kuwa mmoja wa watu walio mjeruhi.
Pia
inadaiwa kuwa Askari huyo aliingia chooni na kufanya mawasiliano na
wenzake huku Madaktari hao wakimsikiliza na kutokana na alichokua
akiongea chooni humo ndipo alipotoka aliambulia kichapo kikali.
Pia
baadhi ya madkatari na wauguzi walikuwa wakisukuma gari alilokuwa
amepanda Dkt Ulimboka huku wakiimba nyimbo za Umoja na Mshikamano Daima
miongoni mwao.
Hali ya ulinzi ilikuwa kali Hospitalini hapo kwani Picha zilikuwa haziruhusiwi kupigwa.
WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2012 WAANZA KAMBI RASMI
Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ni mkurugenzi na muandaaji mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma mbali na kuongeza semina zaidi ili kuwasaidia warembo lakini pia imefanikiwa kuongeza mikoa ambapo mwaka huu wameshiriki warembo kutoka mikoa saba ya Tanzania.
Mbali na kutafuta warembo tu bali Miss Universe ni kama chuo cha kufundisha warembo juu ya kujitambua kama mwanamke na kumpa mbinu mbalimbali za kimaisha.Vilevile mbali na mshindi kupata nafasi ya kutembea nchi mbalimbali za kimataifa pia hutoa fursa kwa mshindi kupata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi kama vile Marekani kwa kupitia mdhamini wetu mkuu New York Film Academy Kambi ya Miss universe Tanzania 2012 imekamilishwa na warembo 20 kutoka mikoa saba ya Tanzania ambayo ni Dodoma, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole sululu, 2009 Illuminata James, 2010 Hellen Dausen na Nelly Kamwelu ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.
Sunday, June 24, 2012
DIANA HUSSEIN ANG’ARA TAJI LA REDD’S MISS DAR INDIAN OCEAN 2012.
Redd’s
Miss Dar Indian Ocean 2012 Diana Hussein (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na Mshindi wa pili Kudra Lupatu (kulia) na Mshindi wa tatu
Zulfa Vuai (kushoto). Shindano la Miss Dar Indian Ocean 2012 limefanyika
ndani ya Kijiji Cha Makumbusho Dar es Salaam.