Pages

Pages

Monday, December 31, 2012

WASHINDI WA UNIQUE MODEL 2012 KWA MATAJI TOFAUTI

Catherine Masumbigana (katikati) akiwa ndiye mshindi wa shindano bora la wanamitindo nchini Tanzania,Unique model 2012 huku mshindi wa photogenic Elizabeth Pertty (kushoto) na mshindi wa kipaji (kulia) Vestina Jax.

Sunday, December 30, 2012

UNIQUE MODEL 2012 MOTO WA KUOTEA MBALI

 Unique model 2012 moja ya event kubwa za mitindo nchini Tanzania,hapa mwanamitindo Zeenath akionyesha uwezo wa miondoko ya kimaonyesho ya nguo.
 Unique models wakionyesha uwezo wa kudansi jukwaani.
Mambo yalikuwa hivi wadau.
 Majaji wakifanya yao.
 Mshindi namba tatu Amina Ayoub akiwapungia watu mkono baada ya ktangazwa.
 Hali ilikuwa namna hii wadau.
 Majaji wakitangaza matokeo.
 Elizabeth Pertty Unique model-Talent 2012 akipungia watu baada ya kutangazwa.
 Mwanamitindo akionyesha kipaji cha kuigiza kwa kutoa ujumbe kuhusiana na gonjwa la ukimwi.
 Unique model of the year 2012 Catherine Masumbigama akipungia mkono mashabiki baada ya kutangzwa kuwa ndiye mwanmitindo wa mwaka 2012-2013.
 Catherine akiwa na Balozi wa shindano la unique model Roseminner.
 Grand finale.
 Vestina Jax Unique model-Talent akifanya yake jukwaani.
 Top five ni Zeeenath Ayoub,Cecilia Emmanuel,Elizabeth Pertty,Catherine Masumbigana na Amina Ayoub.
Mambo yalikuwa hivi wadau.

Saturday, December 29, 2012

CATHERINE MASUMBIGANA ATWAA TAJI LA UNIQUE MODEL OF THE YEAR 2012

Mwanamitindo namba kumi na mbili kiunoni Catherine Masumbigana ameibuka mshindi wa shindano la Unique model 2012 akifatiwa na Cecilia Emanuel huku nafasi ya tatu ikiend kwa Amina Ayoub.


 Mwanamitindo Mwajabu Juma akimvisha taji mshindi wa Unique model- photogenic Elizabeth Pertty baada ya kutangazwa.
Red carpet yetu ilikuwa hivi.
 Balozi wa shindano la Unique model Roseminner akimvisha taji mshindi Catherine Masumbigana baada ya kutangazwa mshindi wa shindano hilo kwa mwaka 2012.

Friday, December 28, 2012

LEO NDIYO LEO NANI KUIBUKA UNIQUE MODEL OF THE YEAR 2012



Ile siku iliyosubiriwa na watanzania wengi kutaka kujua nani ataibuka mshindi wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za pekee nchini Tanzania imewadia
Homa ya shindano imezidi kupanda ikiwa usiku wa leo atajulikana nani atavishwa taji la unque model of the year 2012 taji lenye heshima katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania.
Jumla ya washiriki kumi na mbili wanapanda kujwaani kuwania taji hilo ikiwa fainali zake zitafanyika katika ukumbi wa maraha New Maisha club uliopo Oysterbay jijini Dar.
Wanaowania taji hilo ni Vestina Jax,Judith sangu,Amina Ayoub,Catherine Masumbigana,Elizabeth Pertty,Elizabeth Boniface,Vivian  Gilbert ,Darline Mmari , Zeenath   Habibb,Sandra Suleiman,Cecilia Emmanuel,Magreth Msafiri.
Mratibu wa shindano hili Bwana Methusela Magese amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi siku ya kesho kwani kuna mambo mazuri ya kufurahisha ikiwemo burudani ya muziki wa bendi toka kwa mashujaa,ngoma za asili na bongo flava  kwa kiingilio cha Tshs 15,000/= tu.m

Thursday, December 27, 2012

JOKATE KWA KIDOTI AJIMWAGA UNIQUE MODEL 2012

 Jokate mwongelo kupitia kampuni yake ya Kidoti Loving amejikita ndani ya shindano la wanamitindo lenye mvuto zaidi kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka jijini Dar es salaam.
 Unique models wote watapendeza kwa nywele za Kidoti ambazo zitasukwa kwa ufundi na salon yenye ujuzi wa hali ya juu ya J's professional salon iliopo mnazi mmoja.
 Usikose kuja kutizama wanamitindo wakichuana Live jukwaani desemba 28 ijumaa hii ndani ya New maisha club kule ushuani Oysterbay.
     Thanx Jokate,one Love.

Tuesday, December 25, 2012

ASIA IDAROUS,GYMKHANA HILALL NA MARTIN KADINDA WATEULIWA NA KUTOA UAMUZI UNIQUE MODEL 2012

Baraza la sanaa la aifa limeteuwa majina matatu kati ya sita ya majaji  yaliopendekezwa na  waandaji wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za kipekee.
Uteuzi huo wa wabunfu Asia  Idarous khamsini,Gymkhana Hilall (paka wear) na Martin Kadinda umefanyika mwishoni mwa wiki  hii baada ya baraza la sanaa la Taifa (Basata) kupitia wasifu wao na kuridhika wawe waamuzi rasmi wa shindano la Unique model 2012.
Kinyang’anyiro cha kumsaka mwanamitindo huyo wa mwaka kinajumuisha washiriki kumi na mbili katika jukwaa moja ambapo fainali hizi zitafanyika tarehe 28 desemba katika ukumbi wa maraha New Maisha club ulioko Oysterbay jijini  Dar.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mratibu wa shindano hilo Methuselah Magese amesema kuwa maandalizi ya shindano hilo yako vizuri sana na washiriki wamenorewa kiasi cha kutosha imebaki ni kazi ya umatiwa wapenzi wa mambo ya mitindo kujitokeza kwa wingi kushuhudia nani atachukua taji siku ya ijumaa.
Shindano la unique model litapambwa na burudani toka bendi ya mashujaa ikiongozwa na rapa maarufu Chalz Baba ikiambatana na ngoma za asili toka kwa Costa Siboka na utambulisho wa msanii mkali wa bongo flava B-shop kwa mara kwanza atatoa burudani ambayo haijawahi kutokea.
Magese aliongeza kuwa mbali ya burudani kutakuwa na zulia jekundu(Red carpet) kwa watu maarufu na watu waliopendeza zaidi siku hiyo ambapo kiingilio kitakuwa ni Tshs 15,000 tu kiingilio ambacho hakitengi tabaka la watu flani katika jamii.

Monday, December 24, 2012

BASATA WATEMBELEA KAMBI YA UNIQUE MODEL 2012

 Washiriki wa kinyaang'anyiro cha mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za kipekee uUnique Model 2012 wakipewa semina na afisa toka Basata,tukio hili lilikuwa katika hoteli ya Lamada mwishoni mwa wiki.
Tunaishukuru serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia Baraza la sanaa la Taifa wamekuwa faraja kwetu kutusimamia na kuhakikisha shindano linaendeshwa kwa misingi ya haki na kufuata sheria na ksnuni za mashindano.