Pages

Pages

Wednesday, September 29, 2010

TMG YAFANYA ONYESHO LA MAVAZI ARUSHA

Baadhi ya Warembo wanaounda Kikundi cha 'Tanzania Models Group'


Kikundi cha Wanamitindo wa Tanzania kijulikanacho kwa jina la 'Tanzania Models Group' wanatarajia kufanya onyesho la mavazi katika ukumbi wa Via Via Club jijini Arusha siku ya jumamosi ya tarehe 2,oktoba.

Akizungumza leo, Mratibu wa onyesho hilo lililopewa jina la 'Time and Beauty' Bi. Angel Justace alisema kuwa lengo la kuandaa onyesho hilo ni kuweza kutangaza umoja wao, kuvumbua vipaji vya vijana wenzao na kutangaza Utalii wa nchi ya Tanzania.

Bi. Angel Justace alisema kuwa kwa sasa wakati umefika kwa vijana kuungana katika kutangaza utalii wa nchi.

"Sisi kama vijana hatuna budi kujitoa kwa kuungana na kutangaza Utalii wa nchi yetu, kwani bila kufanya hivyo nchi yetu haiwezi kutambulika na wageni hawawezi kujua nchi yetu ina vivutio gani vinavyovutia,"

Onyesho hilo linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Via Via Club,jijini Arusha siku ya jumamosi ya tarehe 2,oktoba ambapo litawakutanisha wanamitindo kutoka Dar es Salaam na wale wa jijini Arusha huku wakipabwa na mbunifu wa mavazi ya asili Bw. Gabriel Mollel Sairiamu.

Aliongeza kuwa mbali na mbunifu huyo wa mavazi ya asili Bw. Gabriel Mollel Sairiamu pia atakuwepo msanii wa kizazi kipya Hussein Machozi.

Onyesho hilo limedhaminiwa na Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro Conservation-Arusha, Kilimanjaro Express Bus, Mwandago Evestiment,Coco Pazzo, Triple A Radio na Masai Club ya Dar es Salaam.
 

Meneja wa bia ya Balimi Extra,Fimbo Butallah akiongea na waandishi wa habari namna masindano ya mitumbwi yatakavyofanyika katika mikoa ya Mwanza,Kigoma,Mara,Kagera pamoja na Ukerewe katika mkutano na waandishi hao ulifanyika leo makao makuu ya kampuni ya bia Tanzania (TBL).Kushoto ni Meneja msaidizi wa bia hiyo,Edith Bebwa.

Meneja wa bia ya Balimi,Fimbo Butallah (pili shoto),Meneja msaidizi wa bia ya Balimi,Edith Bebwa (shoto) wakiwa na wadau wa Inter grated mara baada ya mkutano huo.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika mkutano huo leo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager leo imezindua rasmi mashindano ya mitumbwi kwa mwaka 2010.

Mashindano hayo ya kupiga kasia, ambayo yatashirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe, yametokea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Akiongea wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Fimbo Butallah alisema, Ni zaidi ya miaka mitano sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki tumefanikiwa kuleta changamoto katika upigaji makasia, kwa kuwapa fursa wapiga makasia kutumia mitumbwi yao katika michezo na kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa lakini pia kuleta burudani kwa wakazi wanaozunguka ziwa Victoria na lile la Tanganyika.

Mashindano haya ya mitumbwi ya Balimi sasa yamekuwa na umaarufu mkubwa na kuongoza kwa mashabiki katika kanda ya ziwa. Kama ilivyo kawaida, mashindano haya yatatanguliwa na burudani mbalimbali za uhamasishaji, zikifuatiwa na mpambano katika hatua ya mwanzo kabla ya fainali kuu itakayofanyikia Jijini Mwanza tarehe 4 Decemba.

Katika hatua za awali mashindano yataanzia Kituo cha Kigoma tarehe 9 Octoba, Kagera 23 Octoba, Mwanza 13 Novemba, Mara na Ukerewe 27 Octoba. Pia ninapenda kuwajulisha washiriki kuwa zawadi za mwaka huu zimeboreshwa zaidi, ukilinganisha na miaka ya nyuma. Hivyo washiriki waongeze mazoezi ili kujihakikishia ushindi katika maeneo yao, pia timu mbili za wanaume na moja ya wanawake zitakazoshika nafasi za juu katika ngazi ya awali ndizo zitakazoingia katika fainali kuu itakayofanyika Jijini Mwanza.

Akizitaja zawadi watakazopata washindi katika ngazi za awali na fainali, Meneja Msaidizi wa Bia ya Balimi Edith Bebwa alisema; Katika ngazi za mikoa zawadi zitakuwa kama ifuatavyo: Ngazi ya Mikoa Fainali Kuu Wanaume Wanawake Wanaume Wanawake

Mshindi wa kwanza 700,000 500,000 2,500,000 2,000,000
Mshindi wa Pili 550,000 400,000 2,000,000 1,500,000
Mshindi wa Tatu 350,000 250,000 1,500,000 750,000
Mashindi wa Nne 300,000 200,000 750,000 500,000
5 hadi 10 - Kila timu 200,000 100,000 400,000 200,000


FAMILIA YA EMANUEL MPANGALA YAMUAGA GENEVIVA KUELEKEA MISS WORLD
 Familia ya Emmanuel Mpangala ikiwa katika picha ya pamoja wakati wa tafrija ya kumpongeza Binti yao Genevieve  aliyeshinda taji la Vodacom Miss Tanzania 2010.Kushoto ni Dunstan na mziwanda Brian. 
 Dua ya kuanza kwa tafrija ikisomwa na babu....
 Wazazi wa Miss Tanzania wakiwa na binti yao.
 Kamati ya Miss Tanzania nayo haipo mbali...
 Burudani ya mziki ikiendelea kutoka kwa ....
 Kalunde Band na hapa Deo Mwanambilimbi akifanya vitu.
 Kocha wa Yanga Papic na Rais Mstaafu wa Klabu ya Yanga Imani Madega wapo...
 Wadau wa TMK wakiongzwa na Ben Kisaka wapo.
 Mambo flani ya sherehe yalikuwa kama hivi Somoe aliongoza msafara huu.
 Miss Tanzania wa zamani (2009) nae huyo anapakua chake...
Mdogo wa Vodacom Miss Tanzania akishusha stata yake

MISS PROGRESS INTERNATIONAL JULIETH WILLY AREJEA TANZANIA NA MAFANIKIO MAKUBWA!!

Miss Progress International Juliet Willy akipozi kwa picha mara alipowasili akitokea nchini Italia alikoshiriki shindano la urembo katika taji hilo na kufanikiwa kutwaa taji hilo la Dunia ambalo ndiyo kwanza limeanzishwa mwaka huu, hivyo kuwatoa kimasomaso watanzania katika nyanja ya Urembo. Juliet amekwa mrembo wa kwanza Tanzania kutwaa taji la dunia katika masuala ya urembo na warembo wengi wameshiriki katika mashindano tofauti tofauti ya dunia lakini bado hawajafanikiwa kufikia katika kutwaa taji la dunia.
Rosemary Momburi Mama mzazi wa Miss Progress International Juliet Willy akimkabidhi ua kama ishara ya kumkaribisha nyumbani Tanzania mara baada ya kufanya vyema na kutwaa taji la dunia linalojulikana kama Miss Progress International.
Miss Progress International Juliet Willy katikati akipungia mashabiki ndugu na jamaa waliokuja kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere jijini Dar es salaam mara baada ya kuwasili akitokea nchini Italia, kulia ni Caroline Sanga Mwandaaji wa Mashindano hayo Tanzania na kushoto ni Rosemary Momburi mama mzazi wa Juliet Willy. 

MSHINDI WA MILIONI KUMI ZA SUPA PESA
Mshindi wa kwanza wa milioni 10 na bahati nasibu ya SUPA Pesa ni Bwana. Khamisi Mohamed Khamisi 32 yrs.
 Amekabidhiwa checque yake leo katika ofisi za Supa pesa.

No comments:

Post a Comment