Pages

Pages

Wednesday, October 20, 2010

Mwanafunzi wa Chuo Aula Milioni Moja Supa Pesa!

Huku droo ya Supa Pesa ikiendelea kutoa mamilioni kwa washindi wake kupitia bahati nasibu inayochezeshwa nchini kote, wikiendi iliyopita imemkuta mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dodoma,tawi la Mwanza, Catherine Nyamoni, akibahatika kujinyakulia kiasi cha milioni moja fedha taslimu.
Mwanafunzi huyo, mwenye umri wa miaka 23, alisema,’ Kweli mimi nilikuwa kati ya watu ambao sitilii maanani michezo ya bahati nasibu wala kuwahi kushiriki kati shindano lolote maishani mwangu. Lakini wiki chache zilizopita nilipokuwa nasikiliza redio nyumbani, nilipata nafasi ya kumsikiliza mshindi wa milioni kumi akipigiwa simu kujulishwa kuhusu ushindi wake. Basi pale ndipo nilipata hamasa kubwa na kuamua kutopitwa na nafasi ya kujaribu bahati yangu. Nilishiriki kwa kutuma ujumbe mfupi kama walivyoelekeza na baada ya kujaribu mara kadhaa nimepata ushindi. Namshukuru Mungu nimefanikiwa na kupata ushindi.’
Catherine aliongezea kusema, ‘ Nitatumia hela za ushindi kuendeleza masomo yangu kwa kununua kompyuta itakayonisaidia kufanya kazi chuoni kwa ustadi zaidi na vilevile hela itakayobaki ninatarajia kutumia kama mtaji wa kuanzisha biashara ndogo ili kujipatia kipato cha kila siku.
Kushiriki droo ya Supa Pesa ni rahisi, inahitaji kutuma ujumbe mfupi wenye neno SUPA kwenda namba 15777. Hii inakuwezesha wewe kuingia moja kwa moja kwenye ushindani wa shilingi milioni moja kila sikui na ukishiriki kutuma Ujumbe mfupi wa simu zaidi ya mara nne basi utakuwa kati ya washindani wa milioni kumi kila w

No comments:

Post a Comment