Pages

Pages

Monday, November 1, 2010

              GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 - SEASON ONE KUZINDULIWA LEO
  Hapo chini,Mbunifu wa
mavazi, Ally Rhmtullah akizungumza katika uzinduzi huo wa shindano la Giraffe Unique Model 2010 linalotarajiwa kuanza na mchakato umefunguliwa leo rasmi,katikati ni meneja wa event katika hoteli ya Giraffe Bwana Gonzaga
 



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhIPpqQIGjsbudiWP6RZ8agM-PxO-yA2a-CnrD6TTkuhrqd6l2fkJlDtjgs1kuNe5OrWiXyt9JQEvIQ4VfqmTZ8UeZZqyoPj6VgFi7mVuss9iKs_tn5tfFJfw5z91d5tmAu8UeDSQzDlN-s/s1600/CIMG0006.jpg

 ali lemtulah na victoria martin majaji wa Giraffe unique mode 2010 - season one
      Kampuni ya Unique Entertainment imeandaa shindano la uanamitindo linalojulikana kama Unique Model 2010 litakalofanyika Desemba 24 mwaka huu katika hoteli ya Giraffe Ocean View. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Unique Entertainment Methuselah Magese alisema kuwa shindano hilo litajumuisha washiriki kumi wa kike.
   Alisema kuwa washiriki hao watapatikana katika mchujo utakaofanyika Novemba 20 mwaka huu katika hoteli ya Giraffe Ocean View. Aliwataja majaji watakaohusika katika mchujo huo kuwa ni mbunifu maarufu wa mavazi nchini Ally Rhemtulla, mwanamitindo Victoria Martin, Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald na mcheza filamu maarufu Steven Kanumba.
    Alivitaja vigezo vitakavyotumiaka katika shindano hilo kuwa ni urefu wa futi 5’ 8’-6’, hips 35-37, kiuno 26-29 na kifua 32-35.Vigezo vingine ni muonekano wa kiuanamitindo, kijiamini na umri 18-25, tabia njema na minato.
   Aliwataka wasichana wenye sifa hizo kujitokeza Giraffe Hoteli Novemba 20 kwa ajili ya mchujo kupata washiriki 20 watakaoingia kambini katika hoteli hiyo Desemba mwaka huu.
                                       vitoria martine

No comments:

Post a Comment