Pages

Pages

Sunday, November 7, 2010

TIMU YA TAIFA YA POOL YAENDA UFARANSA


Mkuu wa wilaya ya kinondoni JORDAN RUGIMBANA akikabidhi bendera ya taifa kwa nahodha wa timu ya pool ALLY AKBAR.
TIMU ya Taifa ya mchezo wa POOL imeagwa rasmi pamoja na kukabidhiwa bendera ya taifa tayari kushiriki kwenye mashindano ya DUNIA ya mchezo huo yaliyopangwa kufanyika nchini UFARANSA.
Wachezaji hao ambao wanaondoka usiku huu waliweza kupata nasaha kutoka kwa mkuu wa Wilaya ya KINONDONI , JORDAN RUGIMBANA ambaye amewataka wachezaji hao kucheza na kuonyesha nidhamu wakati wa mashindano hayo ikiwa ni pamoja na kurudi na ushindi
Naye kocha wa timu hiyo DENIS LUNGU na nahodha ALI AKBAR timu hiyo ipo tayari kushiriki katika mashindano hayo na kuliletea taifa heshma ingwa ni mara ya kwanza kwa TANZANIA kushiriki katika mashindano hayo
Kikosi cha timu hiyo kinajumuisha wachezaji SABA akiwemo mchezaji wa kike pekee VIOLET MREMA ambaye ndiye bingwa wa taifa katika mchezo wa POOL nchini.
Nchi THELATHINI kwa upande wa wanawake na wanaume zinatarajia kutoa wawakilishi wake kushindana katika mashindano hayo ya dunia.

No comments:

Post a Comment