Pages
▼
Pages
▼
Monday, December 6, 2010
WASHIRIKI KUINGIA KAMBINI DESEMBA13 GIRAFFE HOTEL
Washiriki wa shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kitofauti zinazidi kupamba moto siku hadi siku baada ya washiriki kusubiri kwa hamu tarehe ya kuingia kambini kwaajili ya mchuano wa kuwania taji hilo litakalofanyika desemba 24 mwaka huu katika hoteli ya Giraffe hotel iiyopo jijini Dar es salaam.
Jumla ya washiriki kumi watakaoingia kambini ni Ritah samweli,dorah mhando,asia dachi,christina peter,diana hamson,neema silvery,bilkis suleiman,carina suleiman,mariam rabii na caroline makasaka.
Hidaya meeda ndiye matroni wa mamodo hao wakisimamiwa na mwalimu wa dance mkwame mtaalamu wa dance toka chuo cha sanaa bagamoyo .
Giraffe unique model 2010 imedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,global publishers,channel ten,robialac paints,Ali lehmtulah,uniqueentertz blog na Mtaakwamtaa blog.
No comments:
Post a Comment