Pages

Pages

Saturday, January 8, 2011

ALIYEJICHOMA MOTO KUPINGA UKOSEFU WA AJIRA AFARIKI.

Muhitimu wa chuo nchini Tunisia ambaye aliamua kujitoa mhanga kwa kujichoma moto akipinga kukosekana ajira nchi nzima katika taifa hilo la Afrika Kaskazini amefariki dunia.Mohamed Bouazizi (26) alifariki dunia juzi jioni hospitalini nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tunis. Kabla ya kifo chake jamaa huyo alikuwa akiuza matunda na mboga mboga kinyume cha sheria katika mji wa sidi Bouzid baada ya kukosa ajira. Mwezi uliopita aliamua kujimwagia mafuta ya petrol na kujitia kiberiti baada ya polisi kuharibu bidhaa zake kutokana na kutokuwa na kibali maalum.
Zaidi ya watu 5000 walihudhuria Mazishi yake huku waombolezaji wakisema "KWAHERI MOHAMMED sisi tutalipiza kisasi kwa ajili yako. Sisi leo tunalia kwa ajili yako, tutawafanya wale ambao wamesababisha kifo CHAKO WALIE"
Polisi walilazimika kuzuia umati mubwa uliofika nje ya ofisi ya gavana ambako bw. Bouazizi alijilipua. “Muhammad alitoa maisha yake kwa kuonesha uchungu na hali yake na kwa ndugu zake”

Ghasia hizo zimesababisha mwandamanaji mmoja kuuawa baada ya polisi kufyatua risasi

No comments:

Post a Comment