Pages

Pages

Thursday, January 20, 2011

*WAZIRI NCHIMBI AKUTANA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI LEO

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akimuonyesha jarida la Baraza Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi (kulia ). Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) walikuwa na mazungumzo ya kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na taaluma ya habari na waziri Dr. Nchimbi leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo) Raphael Hokororo, akifafanua jambo kuhusu sera ya habari wakati wa mazungumzo kati ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT), na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga. Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Reginald Mengi (kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano huo leo. Kushoto ni Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo. Anayemsikiliza ni Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi .Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao ulioganyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.


WANARIADHA WAPATA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO

                                     Mwanariadha MASUMBUKO akikabidhiwa vifaa vya michezo
                                                          SARAH akikabidhiwa vifaa vya michezo na NCHIMBI
wanariadha wataowakilisha nchi
Hapo jana Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo amekipazia sauti chama cha riadha Tanzania akiwaomba wadhamini binafsi kujitokeza kuusaidia mchezo huo.

Waziri NCHIMBI ametuma maombi haya kwa wadauwakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa wanariadha wawili wa Tanzania watakaoshiriki kwenye mashindano ya riadha ya kimataifa yatakayofanyika huko BAMAKO MALI baadae mwezi huu.

JEASHI LA CONGO 'LILIONGOZA UBAKAJI'

Kamanda wa jeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameshutumiwa kwa kuongoza ubakaji wa wanawake takriban 50 uliofanyika hivi karibuni.Kumekuwa na ripoti nyingi za ubakaji huko Congo lakini tukio hili linaaminiwa kuwa la kwanza kwa idadi kubwa ya wanawake kubakwa likihusishwa jeshi. Mmoja wa waliobakwa, pamoja na vyanzo vilivyonukuliwa katika ripoti ya umoja wa mataifa, wote wanamshutumu Lt Col Kibibi Mutware kwa kuhusika na ubakaji huo uliofanyika mwaka mpya mjini Fizi.

Dr Faise Chacha, mkuu wa hospitali ya Fizi ameeleza, " Askari mmoja aliuawa hapa karibu kabisa na hospitali hii." "Hiyo ilisababisha wasiwasi na wagonjwa wetu wote wakakimbia. Tulirudi siku ya pili asubuhi na tukaanza kuwapokea watu waliokuwa wamepigwa kisu na wengine- wanawake- waliobakwa." Dr huyo na shirika la kitabibu la kutoa msaada Medecins Sans Frontieres wamewatibu waathirika 51 waliobakwa mpaka sasa.

Kama ilivyo kwa matukio ya awali huko Congo, wengi wanatarajiwa kuficha yaliyowasibu kuepuka kuachwa na waume na familia zao. Wawili miongoni mwa wanawake hao walikubali kuzungumza na BBC ilimradi tu wasitajwe majina yao.

Mmoja aliiambia BBC, " Nilibakwa mbele ya watoto wangu wanne." "Ninaona aibu, ninaona aibu sana. Nikikutana na watu wawili au watatu ambao wanajadili jambo, naanza kuhisi tu kuwa wananizungumzia mimi, hata kama si kuhusu mie."

Mwanamke huyo mwengine alifanikiwa kumtambua aliyembaka. "Ilikuwa jioni na walionibaka walikuwa wanajeshi," alisema kwa sauti ndogo, mwili wake ukiwa umefunikwa na khanga yenye rangi za kuvutia. nakuongeza kwa kusema " Walikuwa wanne- Kibibi na walinzi wake. Wameiba vitu vyetu vyote pamoja na pesa."


TAIFA STARS YALAMBA MILIONI 75

WAANDAAJI wa michuano ya soka kwa Nchi za Bonde la Mto Nile wameipa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' sh.milioni 75, ingawa ilivurunda.

Taifa Stars ilishika nafasi ya sita kati ya timu saba zilizoshiriki mashindano hayo ya kwanza ambayo yameandaliwa na Misri,huku Burundi ikiwa ndiyo ya mwisho na Sudani imeshika nafasi ya tano, baada ya Jumapili kuifunga Taifa Stars mabao 2-0 katikamechi ya kuwania nafasi ya tano.Lakini juzi Taifa Stars, Sudani na Burundi timu vibonde katika mashindano hayo zilitangazwa kila moja kupewa dola za Marekani50,000 sawa na sh. milioni 75 za Tanzania. Mashindano yaliandaliwa na Chama cha Soka cha Misri (EFA).

Fedha hizo ziliztangazwa baada ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Jeshi mjini hapa ambapo Misri iliibuka naushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uganda na kuibuka bingwa.

Kwa kutwaa ubingwa huo ambao unaifanya Misri kuwa bingwa wa kwanza ilizawadiwa dola 150,000 za Marekani sawa na sh. milioni225 za Tanzania, wakati Uganda iliyoshika nafasi ya pili ilizawadiwa dola za Marekani 120,000 sawa na sh.milioni 180 zaTanzania.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambayo juzi iliifunga Kenya baop 1-0 ma kushika nafasi ya tatu, yenyewe ililamba dolaza Marekani 100,000 sawa na sh. milioni 150 za Tanzania, huku Kenya yenyewe ikitia kibindoni dola 60,000 sawa na sh.milioni90 za Tanzania.

Dola moja ya Marekani kwa sasa ni kati ya sh.1460 hadi 1500 hivyo kuifanya angalau Taifa Stars nayo kupoza machungu ya kukosazawadi kubwa za mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

Taifa Stars ambayo haikushinda mechi katika mechi ilitarajiwa kuondoka jana usiku na kufika Dar es Salaam leo alfajiri ikiwa,ikiwa imefungwa mechi mbili na kutoka sare mbili Ilifungwa na Misri mabao 5-1, ilifungwa na Sudani mabao 2-0 na ilitoka sare ya bao 1-1 na Uganda na sare kama hiyo na timuiliyoshika nafasi ya mwisho Burundi, ambayo ilipata pointi moja tu ya Stars.

Wakati huohuo, kipa Kidiaba wa DRC alitangazwa kuwa Kipa Bora wa Mashindano, huku mshambuliaji Said Khamdi wa Misri ambayemechi ya fainali alifunga mabao mawili alitangazwa kuwa Mfungaji Bora baada ya kufunga mabao sita na Ahned Said Faraj pia waMisri aliibuka Mchez
aji Bora.

No comments:

Post a Comment