Pages

Pages

Tuesday, January 25, 2011

KASHFA NZITO YAIBUKA MWAUWASA: MILIONI 340 ZATAFUNWA NA WAJANJA.

Bodi ya mamlaka ya maji na maji taka jijini Mwanza (MWAUWASA) imeonyeshwa kuchukizwa na upotevu wa shilingi milioni 340 na imekusudia kutomuongezea muda wa mkataba Mkurugenzi wake Justus Rwetebula baada ya kuelekea kumalizika .HUDUMA YA MAJI NYUMBA ZA VILIMA VYA mwanza.

Mmoja kati ya wajumbe ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kuwa kwa ujumla Bodi imechukizwa na namna Mkurugenzi huyo alivyoshindwa kutoa taarifa kwa Bodi juu ya wizi huo uliofanywa na mhasibu wa MWAUWASA Moses Ndaki.

“Mara baada ya wizi huo kutokea Mkurugenzi aliamua kwenda likizo na kumwachia maelezo nusunusu aliyemwachia ofisi, unaweza kuona ni namna gani Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA asivyo makini na kazi yake ndiyo maana wajumbe wa Bodi kwa kauli moja tumeamua kutokumwongezea muda wa kazi baada ya kipindi chake kumalizika hivi karibuni wakati hatua nyingine za kiutendaji zikichukuliwa na mamlaka husika ambazo zimepewa jukumu la kuchunguza wizi huo na kuchukua hatua” alisema mjumbe.

Mjumbe huyo ameongeza kuwa kuna mtandao mkubwa wa wafanyakazi uliofanikisha wizi huo kwani fedha hizo inaonyesha zilikuwa zikiibiwa kwa awamu huku baadhi ya viongozi wakiwa kimya wakijua mchezo
.

Kwa upande wake Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Nonosius Komba amesema kuwa jeshi lake bado linamsaka mhasibu Moses ndaki aliyedaiwa kutoweka kazini baada ya kubainika wizi huo wa milioni 340.

Komba ameongeza kwa kusema kuwa polisi pia kwa kushirikiana na uongozi wa MWAUWASA bado wanachunguza kwa makini tukio zima ili wahusika waweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma za wizi huo.

No comments:

Post a Comment