Pages

Pages

Friday, January 21, 2011

Mawaziri Tunisia wajitoa chama cha RCD

Televisheni ya taifa imeripoti, mawaziri wote katika serikali ya mpito ya Tunisia ambao walikuwa katika chama cha Rais aliyekimbia, RCD, wamejitoa kwenye chama hicho.
Hata hivyo, mawaziri hao wataendelea kushikilia nafasi zao za uwaziri katika serikali ya umoja wa kitaifa.
Hapo awali, ilitangazwa kuwa zaidi ya wanachama 30 wa familia ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo walikamatwa.
Maandamano Tunisia
Maandamano Tunisia
Wakati hali Tunisia ikizidi kuwa tete, majeshi yalifyatua risasi za kutoa tahadhari wakati waandamanaji walipoendelea kuzunguka mjini Tunis.
Taarifa kutoka eneo hilo zinaeleza kwamba baadhi ya waandamanaji walijaribu kupanda ukuta wa makao makuu ya RCD.
Majaji wa Tunisia nao waliandamana Tunis wakitaka majaji wote waliofanya kazi chini ya Rais aliyekimbia wajiuzulu.
Vile vile kumekuwa na taarifa za kuwepo maandamano siku ya Alhamis katika miji ya Gafsa na Kef.
Rais Zine al-Abidine Ben Ali alikimbilia Saudi Arabia wiki iliyopita baada ya kufanyika maandamano makubwa ya kupinga ukosefu wa ajira, umaskini na rushwa.
Licha ya kuondoka, maandamano yamekuwa yakiendelea, huku waandamanji wakitaka wanachama wote wa RCD waondoshwe madarakani.
Mawaziri wanne kutoka upinzani wameng'atuka kutoka baraza la mawaziri la serikali ya mpito siku moja baada ya kuundwa, wakitaka mawaziri kutoka chama cha RCD wasihusishwe.
Waziri mkuu Mohammed Ghannouchi na Rais wa serikali ya mpito Fouad Mebazaa- aliyekuwa spika wa bunge dogo- nao wamejiondoa kwenye chama cha RCD ili kujaribu kujiweka mbali na Bw Ben Ali.

Muuaji wa wanawake afungwa Afrika kusini

Thozamile Taki
Thozamile Taki
Muuaji kutoka Afrika kusini amehukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la kuua wanawake 13.
Thozamile Taki, mwenye umri wa miaka 40, anayejulikana kama 'sugarcane killer' kutokana na kutupa miili ya wanawake hao kwenye mashamba ya miwa, na kuwalagahi kwa kuwaahidi kuwatafutia kazi.
Akimhukumu Taki kifungo cha maisha kwa kila kesi, Jaji King Ndlovu amemwelezea kama "mbweha kwenye ngozi ya kondoo."
Raia wa Afrika kusini wamefurahishwa na hukumu hiyo na kusifu jitihada za polisi.
Ndugu wa marehemu- baadhi ambao walikuwa wakimjua Taki binafsi-walilia na kushangilia wakati Jaji Ndlovu alipokuwa akisoma hukumu hiyo katika mahakama kuu ya Durban siku ya Jumatano mchana.
Jaji Ndlovu alisema, jinsi Taki alivyokuwa wakati wa kesi hiyo imechangia katika kutoa uamuzi wa kifungo hicho.
Alisema, " Hata waathiriwa walipolia hadharani wakati wa kutoa ushahidi, ulitabasamu tu."
Zaidi ya watu 100 walitoa ushahidi dhidi ya Taki wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa mwaka 2009.
Miili ya wanawake hao iliyokuwa imeoza ilipatikana kwenye mashamba makubwa ya miwa na chai huko Umzinto, KwaZulu-Natal na Port St Johns mwaka 2007.
Taki amenyimwa haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu yake hiyo na anatarajiwa kupelekwa kwenye gereza lenye ulinzi wa hali ya juu huko KwaZulu-Natal.


 WANANCHI WA  MBEYA WATEKETEZA BASI KWA MOTO

               IGP Mwema
Wananchi wanao daiwa kuwa na hasira kali wakazi wa wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wameteketeza basi kwa moto baada ya basi hilo kumgonga mtembea kwa miguu.
Akizungumza kwa njia ya Simu Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Advotece Nyombi, alisema kuwa pamoja na wananchi hao kuchoma moto basi hilo bado wameweza kufunga barabara na kupelekea msongamano mkubwa wa magari katika eneo hilo la tukio.
Alisema kuwa tukio hilo limetokea leo na kuwa hadi sasa jeshi la polisi linaendelea na jitihada za kuwasihi wananchi hao kutuliza jazba ili kufungua barabara hiyo.
Kamanda huyo alisema mbali ya mtu mmoja huyo aliyegongwa na basi hakuna mtu mwingine ambaye amepata kufa wala kujeruhiwa katika tukio hilo.

Blacks and greys dominate Milan men's catwalks

 Greys and blacks dominated the catwalks Tuesday as Giorgio Armani, DSquared2 and Neil Barrett wound up the fourth and last day of the Milan's men fashion shows for autumn-winter 2011-2012.

Armani presented grey in all its incarnations -- stone coal, blue-grey, greyish-green, with jackets with strong shoulders and clean silhouettes.
Overcoats and fur-lined leather coats, coloured shirts in violet, pink and orange, and buckskin shoes rounded out the collection.
As was to be expected, the twin stylists of DSquared2 put on a spectacular show, complete with a "Little House on the Prairie"-style covered wagon.
The Wild West atmosphere was reflected in the mainly black clothes, with black Wyatt Earp hats and leather braces.
The duo's jackets were very long and tied at the waist with a belt, or very short and hyper-cinched.
Jeans were worn low on the waist, while for nights out there were little waistcoats with khaki on the front and tartan in the back.
In terms of materials, flannel, wool and leather dominated.


USAWA WA KIJINSIA UTAFIKIA HAPA SASA...!!!
Kelele za wanajinsia kutaka usawa wa 50 kwa 50 kati ya mwanamke na mwanaume unaendelea kupata mafanikio makubwa lakini itafika siku wanawaqke wadai haki zote za matendo ya mwanaume mfano kamili ni hapa juu...cheki mdada anavyoinjoi kutoa taka mwili as man....teh  teh...malengo ya milenia ..to empower women.......,vijimamboz 


PRECISION AIR KULETA MAPINDUZI YA BEI ZA NAULI YA NDEGE
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNfKuxAlj3p5EUm-YHVdS-W4RY6e5MGrcVCTBlEVjHyN454XQLHGU9_rsPiCdfeHmgG2gh7I9zsyEZO_qoDP9OssjOFwSeQ6sT_wfRSo3qzwLHH-9nIgptbSOUfBlQxr6Nu2maphsGWUo_/s1600/mwaki.jpg  Nauli ya kwenda Zanzibar kuwa 35,000/=, na ukikata ya kwenda na kurudi 60,0000/= Kwa muda wa miezi mitano,akizungumza na waadnishi wa habari mkurugenzi biashara phili mwakitawa 

No comments:

Post a Comment