Pages

Pages

Tuesday, January 18, 2011

MCHEZO WA BAO WAPATA VIONGOZI

Rais wa shirikisho la mchezo wa bao katikati MONDAY LIKWEPA pamoja na wajumbe  \

Baada ya kutokea kwa simtofahamu katika chama cha mchezo wa bao kutoka na kutokuwa na viongozi wanotambulika na Baraza la michezo nchini Taifa limeteuliwa viongozi wapya wa kuendesha mchezo huo.

Akijitambulisha mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti mpya wa shirikisho la mchezo wa boa TANZANIA (SHIMBATA) MONDAY LIKWEPA amesema kuwa wafurahi kuundwa kwa shirikihso hilo ambalo mchakato wake umechukua muda mrefu mpaka kukamilika.

Likwepa amesema kuwa shirikihso hilo limesajiliwa  na baraza la mcihezo nchini BMT  ambapo amesema wanatarajia  kuanza michezo ya ndani na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment