Pages

Pages

Monday, January 31, 2011

    TIDO MHANDO KUTUPIWA ZENGWE JINGINE
BAADA ya kung’olewa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando amekumbwa na msukosuko mwingine kutokana na baadhi ya wanachama wa Chama cha Maendeleo Muheza (MDTF) kutaka sekretarieti ya chama hicho kujiuzulu. sasa.
Wanachama hao wametaka sekretarieti hiyo ing’oke kutokana na kudaiwa kushindwa kuleta maendeleo katika kipindi cha miaka miwili, hivyo kuhatarisha uhai wa chama hicho.
Kwa mujibu wa kundi hilo, wanachotaka ni uongozi wote wa sasa kujiuzulu, kwani uongozi uliopita ulifanikiwa kuleta maendeleo ikiwamo ujenzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari Muheza, ujenzi wa visima vya maji na Shule ya Sekondari Kelenge.
Walisema kasi ya ukuaji wa chama haionekani tangu kuingia madarakai sekretarieti mpya.
Akizungumzia suala hilo jana jijini Dar es Salaam, msemaji wa chama hicho, Ramadhan Semtawa, alikiri kuwapo kwa mpango huo wa mapinduzi.
“Ni kweli huo mpango wa mapinduzi nimeusikia. Jana nimezungumza na mkurugenzi anasema Tido yuko Uingireza na amepanga tukutane karibuni.
“Ninachosema sekretarieti haijashindwa kazi na sioni sababu ya kujiuzulu. Tunaomba utulivu kwani mipango inatekelezeka. Saccos tayari iko chini ya Mama Semainda ambaye alikuwa Mkurugenzi wa BoT, tawi la Mwanza.
“Tatizo mwaka jana kulikuwa na mambo ya uchaguzi, ila tutajitahidi na Balozi Adad Rajabu yupo kwa sasa atatupa mbinu,” alisema.
Katika sekretarieti cha chama hicho, Tido ni Mwenyekiti, Mary Chipungahelo (Makamu Mwenyekiti), Nehemia Mchechu (Mhazini), Albert Semng’idu (Katibu), Clement Mang’enya (Mkurugenzi Mtendaji) na Ramadhan Semtawa (Katibu Mwenezi).
Sekretarieti hiyo iliingia madarakani baada ya kuondoka uongozi chini ya uenyekiti wa Balozi Adad.
Hata hivyo, Semtawa kwa upande wake, alisema kama shinikizo hilo litaongezeka atajiuzulu kabla ya kutokea kwa mapinduzi.
“Shikinizo likiongezeka nitajiuzulu kabla ya mapinduzi,” alisema Semtawa.


MFANYAKAZI SHUPAVU WA GIRAFFE HOTEL AFARIKI DUNIA
   Mr.Gonzaga (mwenye suti katikati) enzi za uhai wake katika press conference ya uzinduzi wa unique model 2010.kulia kwake ni magese na kushoto kwake ni lehmtulah

Meneja ukumbi na matukio wa hoteli Giraffe ocean view ya jijini Dar es saalam amefarki dunia usiku wa kuamkia jana kwa ajali ya pikipiki,kifo chake kimestua wengi hususani mkurugenzi wa hoteli Bwana Charles Bekoni na wafanyakazi wa Giraffe hoteli.
  UNIQUE eNTERTAINMENT imesikitishwa sana na msiba huu kwani Bwana Gonzaga tumekuwa nae sambamba katika mchato mzima wa Unique model.

    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU GONZAGA

No comments:

Post a Comment