Pages

Pages

Monday, February 21, 2011

ROSTAM AZIZI AITESA TANZANIA!!!....??

Mh.Rostam Aziz ametajwa na mmiliki wa DOWANS kuwa alikuwa anahusika na kampuni hiyo kwa namna moja ama nyingine kwamba alikabidhiwa kuiongoza dowans Tz.

  Kiinimacho hiki kimejitokeza mwishoni mwa wiki hii baada ya mliki wa DOWANS kujitokeza kutoka Oman na kudai kuwa yeye ndiye mliki wa kampuni hiyo akiwa na hisa nyingi zaidi wakati jina lake halipo katika usajili wa kampuni na katika majina aliyotaja Mh.Ngereja halikuwamo la Mohammed yahya.

  Hii ni kuwatania watanzania wengi wenye uchungu na nchi yao kwani kama Mh rosta alijua anahusika kwanini alinyamaza kimya na kusumbua akili za mamilioni ya watanzania.

  Inamaanisha ripoti ya Mh. Mwakyembe ni ya uongo!? jamani hata waziri ista anaweza kuidanganya umma..? hatuamini sana kauli ya huyo mwarabu.

  kuna umuhimu wa viongozi wa ngazi za juu kuchukua hatua za haraka kupoza hasira za watanzania wengi kwa kuweka mambo bayana, na hapo ndipo watanzania wengi watakumbuka sera za Mch.Mtikila.


Rais Yoweri Museveni ashinda kwa kishindo!

Tangazo rasmi limetolewa kuthibitisha kuwa Rais Museveni ndiye mshindi katika uchaguzi uliofanywa Ijumaa.
Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni
Tume ya uchaguzi ilitangaza kuwa Yoweri Museveni alishinda kwa asilimia 68, katika uchaguzi huo uliofanyika Ijumaa, naye mpinzani wake mkuu Kizza Besigye alipata kura asilimia 26.
Bw Besigye amekataa kukubali matokeo hayo na kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika shughuli ya uchaguzi.
Chama kilicho madarakani kimetuhumiwa kwa kutumia rasilmali ya serikali kuwahonga wapigaji kura.
Uchaguzi huo uliendelea kwa utulivu ingawaje kuna ripoti za vurugu kadhaa baina ya wafuasi wa chama kinachotawala na chama cha upinzani.



 FEDHA MPYA ZAZAGAA MJINI MBEYA
    BENNO NDULU GAVANA WA BENKI KUU TZ
 Noti feki mpya zimeonekana kuzagaa kwa kasi ikiwa ni muda mchache tu toka kutolewa kwa noti hizo mpya na benki kuu ya Tanzania,katika mjii wa mbeya si kitu cha kushangaza kwani inaonekana wazalishaji wa noti hizo bandia wako huko.
  Hujuma hizi zinaurdisha nyuma uchumi wa nchi na kufanya mzunguko wa fedha kudorora na kuipa serikali hasara ya kuchapa pesa nyingine kwani wananchi bado hawajapewa elimu ya kutosha jinsi ya kuzitofautisha zipi halali na zipi feki,ikiwa hivi majuzi tu noti feki kibao zilikamatwa jijini mwanza.

Watu 250 wauwawa Libya

Shirika la kugombea haki za kibinaadamu, Human Rights Watch, linakisia kuwa watu zaidi ya mia mbili hamsini wamekufa katika siku chache za fujo za Libya.
Waandamanaji wanaotaka Gaddafi aachie madaraka
Waandamanaji wanaotaka Gaddafi aachie madaraka
Taarifa kutoka Libya zinaeleza kuwa hali katika mji wa Benghazi ni ya kutisha, siku moja baada ya bunduki za rashasha na silaha kubwakubwa kutumiwa dhidi ya watu waliokuwa kwenye mazishi.
Walioshuhudia matukio ya jana walisema kulikuwa na mtafaruku wakati wanajeshi wa Libya, waliokuwa juu ya mapa, waliwalenga na kuwafyatulia risasi waombolezajii waliokuwa kwenye maziko ya mwandamanaji aliyeuliwa na askari wa usalama.
Daktari mmoja aliiambia BBC kwamba watu wengine waliuwawa mbele ya nyumba zao, na kwamba mahospitali yamejaa maiti.
Maelfu ya raia katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo wamekuwa wakiandamana kuipinga serikali ya nchi hiyo amabayo imekuwa chini ya uongozi wa Kanali Muammar Gaddafi kwa miongo minne sasa.
Waandamanaji walioko Marekani wakiwaunga mkono raia wa Libya
Waandamanaji walioko Marekani wakiwaunga mkono raia wa Libya
Kambi ya upinzani imesema shambulio hilo si halali kwani askari hawakuchokozwa lakini kikosi cha usalma kinadai kuwa baadhi ya waandamanaji waliwarushia mabomu.
Libya ni mojawapo ya nchi za kiarabu ambazo zimekumbwa na maandamano baada ya raia wa nchi za Tunisia na Misri kuandamana na kuwalazimisha marais wa nchi hizo kujiuzulu.
Rais wa Tunisia Zine El Abidine Ben Ali aliikimbia nchi yake Januari mwaka huu naye rais Hosni Mubarak wa Misri alijiuzulu Februari 11.


KEISHIA DIOR: MSICHANA MWENYWE MACHO MAZURI KWA MWAKA 2010
 Angalia jicho la mtoto wa kijamaica,she is star,model,actress,ect...shez sexy enough

vurumai yazuka Morocco

Maelfu ya waandamanaji wamejumuika mjini Rabat Morocco kudai kuwa Mfalme Mohammed,agawe sehemu ya madaraka yake.
Mfalme wa Morocco, Mohammed
Mfalme wa Morocco, Mohammed
Ripoti zinasema polisi wamesimama mbali na waandamanaji katika maandamanao yaliyoanzia kwenye mlango wa mji wa kale kuelekea majengo ya bunge.
Polisi hawakuwasumbua waandamanaji walipokuwa wakikaribia jengo la bunge wakiimba 'hatuitaki katiba ya utumwa'.
Kuna maandamano mjini Casablanca nchini humo na mengine yamepangwa kufanywa Marrakesh.
Maandamano ya Jumapili yalipangwa na makundi mbaliimbali ikiwemo kundi linaloijiita Kundi la mabadaliko ya Februari, "The February Movement for Change", ambao una mvuto kubwa zaidi kwenye mtandao wa kijamii wa intaneti, Facebook.
'Haya ni maandamano yasiyo na vurugu na ni ya kuishinikiza serikali ibadili katiba na kuwa inayoheshimu binadamu na kutokomeza ufisadi,' alisema Mustapha Muchtati kutoka kundi la Baraka, mojawapo ya makundi yanayoandaa maandamano hayo.
Waziri wa Fedha wa Morocco Selaheddine Mezouar amewahimiza raia kuacha maandamano, akisema kuwa endapo maandamano haya yatachochea vurugu zaidi nchi hii itapoteza utulivu na imani, tuliyojenga katika kipindi cha muongo moja, katika siku chache tu.'
Wadadisi wanasema, katika nchi za Kiarabu zilizokumbwa na maandamano ya raia, Morocco ni tofauti kwani ina uchumi uliostawi, wabunge waliochaguliwa na wananchi na ufalme unaoleta mabadiliko; kwa hivyo maandamano huko hayatoshika kasi.

No comments:

Post a Comment