Pages

Pages

Wednesday, February 2, 2011

Ghasia zaongezeka Misri

Wafuasi wa Rais wa Misri, Hosni Mubarak wamekabiliana na waandamanaji wanaomtaka kiongozi huyo aondoke madarakani katikati mwa mji wa Cairo.
Wafuasi na wapinzani wa Mubarak wakipambana
Wafuasi na wapinzani wa Mubarak wakipambana
Maelfu ya wafuasi wa Bw Mubarak walimiminika kwenye eneo la Tahrir na kuondoa vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na waandamanaji.
Pande hizo mbili zilirushiana maneno kabla ya kuanza kurushiana mawe.
Jeshi ambalo awali lilitoa wito kwa waandamanaji kutawanyika na kurejea katika shughuli zao za kawaida bado halijaingilia kati.
Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinasema maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia kiraia walikuwa miongoni mwa baadhi ya wafuasi wa Bw Mubarak waliojitokeza katika eneo la Tahrir.
Mapambano mengine yameripotiwa kwenye mji wa Alexandria.


KIGOGO ALIEITAFUNA TANESCO MATATANIMHASIBU wa Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), Lilian Chengula, amepandishwa kizimbani mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akidaiwa kuiba fedha za shirika hilo sh bilioni 1.3.
Aidha mshtakiwa huyo alisomewa mashitaka 85 jana mbele ya hakimu Mustapha Siani na moja kati ya mashitaka hayo likiwa la uhujumu uchumi na yaliyobaki ya wizi.
Chengula alidaiwa kutenda makosa hayo kati ya mwaka 2009 hadi Septemba 2010 katika ofisi za shirika hilo wilaya ya Kinondoni, akitumia wadhifa alionao.
Ilidaiwa na waendesha mashitaka, Zuberi mkakati, Inspekta wa polisi Ema Mkonyi na Beatrice Mpangala waliosoma mashitaka hayo kwa kupokezana kuwa Chengula alikuwa akiliibia shirika hilo kwa kutumia vocha alizokuwa akiziwakilisha kwa nyakati tofauti.
Katika shitaka la uhujumu uchumi, mshitakiwa alidaiwa kusababisha hasara kwa mamlaka iliyowekwa kisheria ambayo ni mwajiri wake Tanmesco Sh 1,312,717,717.70 kinyume cha sheria ya uhujumu uchumi.
Mshitakiwa alikana mashitaka yote isipokuwa la uhujumu uchumi ambalo mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza isipokuwa kwa kibali toka kwa mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP), mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina kibali cha kusikiliza kesi hiyo.
Mahakama hiyo itatoa maamuzi juu ya dhamana ya mshitakiwa kesho baada ya mwendesha mashitaka kuiomba mahakama isimpe dhamana kwa madai kuwa haina uwezo wa kusikiliza moja ya mashitaka yanayomkabili na ipuuze maombi ya mshitakiwa ya kutaka apewe dhamana.


15 wakamatwa Sudan wakipinga bei kupanda

Takriban waandamanaji 15 wamekamatwa katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum katika kile ambacho wanaharakati wanasema ni maandamano ya kupinga kupanda bei za bidhaa katika miji mingine.
Maandamano Sudan
Maandamano Sudan
Zaidi ya watu 100 wametiwa mbaroni hadi sasa tangu kuanza maandamano hayo siku ya Jumapili, kwa mujibu wa kikundi kinachotetea haki za binaadamu, Africa Centre for Justice and Peace Studies .
Polisi wanakanusha taarifa kwamba mwanafunzi mmoja aliuwawa katika maandamano mapema wiki hii.
Waandishi habari wanasema inaelekea maandamano hayo yametayarishwa kupitia tovuti, yakihamasishwa na matukio ya Tunisia and Misri.

Siku ya Jumanne waandamanaji kadhaa walikusanyika katika uwanja wa Jackson Square, mojawapo ya vituo vikuu vya basi mjini Khartoum, pale vikosi vya usalama vilipowavamia na kuwatia mbaroni watu kadhaa waliokuwepo hapo.
Wakereketwa wanaotetea haki za binaadamu wanasema idadi ya watu waliokamatwa huenda ikafika 30.
Wanahisi huenda ulikua mtego wa vikosi vya usalama ambavyo walivishutumu kwa kuweka ujumbe kwenye mtandao wa Facebook kuwataka watu washiriki katika maandamano.
Mwaandishi wa BBC James Copnall akiwa mjini Khartoum anasema kulikua na maandamano mengine siku ya Jumanne usiku mjini Khartoum na mji pacha wa Omdurman.
Maandamano hayo yametayarishwa zaidi na wanafunzi na yamedhibitiwa zaidi katima maeneo ya vyuo vikuu.

No comments:

Post a Comment