Pages

Pages

Monday, February 28, 2011

NH.CHEYO ANAPENDA KUBANJUKA..!!


Mbunge wa UDP Bwana John cheyo inasemekana anaupenda sana wimbo wa DNA uitwao "banjuka".

  Cheyo wakati akihojiwa na redio moja hapa nchini alipoulizwa je anapenda muziki gani alitoa kauli ya kuduwaza wengi kuwa anapenda wimbo mmoja tu wa banjuka.

 

Waziri mkuu wa Tunisia ajiuzulu

Tunisia

Waziri mkuu wa Tunisia Mohammed Ghannouchi ametangaza kupitia televisheni ya taifa kuwa anajiuzulu- matakwa muhimu kutoka kwa waandamanaji.
 Alikuwa akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Tunis, baada ya kutoa hotuba ndefu akijitetea wakati alipokuwa madarakani
 Bw Ghannouchi anaonekana kuwa karibu sana na aliyekuwa Rais Zine al-Abidine Ben Ali, aliyeondoshwa madarakani mwezi uliopita.

Bw Ghannouchi, mwenye umri wa miaka 69, amekuwa chini ya uongozi wa Bw Ben Ali tangu mwaka 1989.

Alisema, " Baada ya kutafakari kwa zaidi ya wiki moja, nikaanza kushawishika, na familia yangu iliniunga mkono, na hivyo kuamua kujiuzulu. Si kwamba nakimbia majukumu yangu; nimekuwa nikitimiza wajibu wangu tangu Januari 14

Misri yamzuia Bw Mubarak kusafiri


Bw Hosni Mubarak
Mwendesha mashtaka wa Misri ametoa hati ya kumzuia Rais aliyeondoka Hosni Mubarak kusafiri pamoja na familia yake.
Msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka alisema amri hiyo pia inapiga tanji fedha na mali zao.
Bw Mubarak aling'atuka Februari 11, baada ya kukaa madarakani kwa takriban miaka 30, kufuatia kuibuka maandamano yaliyofanywa na umma ukimpinga.
Inaarifiwa kuwa afya yake ni duni, akiishi kwenye nyumba yake ya kifahari huko Sharm el-Sheikh, lakini hajaonekana wala kusikika hadharani tangu alipoachia madaraka.
Alikabidhi uongozi wake kwa jeshi, ambapo iliteua serikali ya mpito itakayoandaa katiba mpya na uchaguzi pia.
Shirika la habari Reuters limeripoti kuwa ofisi ya mwendesha mashtaka alisema kizuizi hicho cha kusafiri na kupiga tanji mali zake ilitolewa wakati malalamiko yalipotolewa- ambapo haijfafanuliwa- dhidi ya familia ya Bw Mubarak wanachunguzwa.
Misri tayari imeziomba serikali kadhaa kupiga tanji mali za familia ya Bw Mubarak nje ya nchi.
Waandamanaji pamoja na wanaopinga ufisadi wamekuwa wakishinikiza mali za familia ya Bw Mubarak zichunguzwe, ambayo inakadiriwa kuwa kati ya dola za kimarekani bilioni moja hadi bilioni 70.
Hata hivyo, mwakilishi wa kisheria wa Bw Mubarak amekanusha taarifa kuwa aliyekuwa Rais alijilimbikizia mali akiwa madarakani.

 ARSENAL YALAMBWA 2-0

 Birmingham City imeshangaza wengi kwa kuichapa Arsenal 2-1 katika fainali ya Kombe la Carling.

Martins
Obafemi Martins baada ya kupachika bao la ushindi
Arsenal, waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya ushindi katika mchezo huo kwenye uwanja wa Wembley, walishindwa kutumia fainali hii kumaliza ukame wa vikombe katika klabu hiyo.
Nicola Zigic wa Birmingham aliandika bao la kwanza katika dakika ya 28, kufuatia mpira wa kona kupigwa.
Wenger
Arsene Wenger
Nahodha wa Arsenal katika mchezo huo Robin Van Persie akiongoza kwa mifano, alisawazisha bao hilo dakika sita kabla ya mapumziko.
Arsenal waliendelea kulisakama lango la City, lakini kipa Ben Foster alisimama imara hasa kwa kuzuia mikwaju ya Samir Nasri na Niklas Bendtner.
Mambo yalibadilika wakati mashabiki wakidhani huenda mchezo ukaenda katika dakika za nyongeza.
City
Alex McLeish, kocha wa City
Bao la ushindi la City lilipatikana katika dakika ya 89 baada ya kipa wa Arsenal Wojsiech Szczesny na beki wake Laurent Koscielny kujichanganya na kumpa nafasi Obafemi Martins kufunga bao aliloliita jepesi zaidi maishani mwake.
Ushindi huu unaipa nafasi City kucheza Ulaya msimu ujao. Mara ya mwisho Birmingham kushinda ushindi kama huu ilikuwa mwaka 1963.
Mara ya mwisho kwa Arsenal kunyakua kombe muhimu, ilikuwa mwaka 2005.

 
KIM KARDASHIAN AFURAIA KUPIGA PICHA ZA UTUPU
Mwanamitindo maarufu duniani kim kardashiani ameingia lawamani baada ya kupiga picha akiwa mtupu kwaajili ya gazeti la W,Aidha kim amefurahishwa na kitendo hiko kwakua kimemuongezea usuper-staa zaidi.


 ELIZABETH NA KELVIN WAFUNGA NDO

Mshindi wa dola 200,000 za Big Brother Africa 4-The revolution iliyofanyika mwaka 2009,Kelvin Chuwang Pam aka Shemeji toka pande za Jos Plateau-Nigeria amefunga ndoa na housemate mwenzake wa Big Brother Africa 2009 toka TZ,Elizabeth Gupta kwenye sherehe ya harusi iliyofanyika jijini Lagos-Nigeria.
Kelin na Elizabeth wameweka historia ya kuwa housemates wa kwanza walioshiriki Big Brother Africa kufunga ndoa,acha engine walioishia kuchakachuana kwenye jumba hilo....Big Up,tunawatakia ndoa njema

 WATANZANIA WACHEMSHA MBIO ZA MARATHON 2011
Washiriki wa mbio hizo wakianza kutimua mbio baada ya kuanzishwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Moshi.

Jaribio la mapinduzi lazimwa Congo

Habari kutoka Kinshasa zinaeleza kuwa watu saba wameuawa baada ya kufanya jaribio la kumpindua Rais Joseph Kabila katika makazi yake.
Watu hao waliuawa na walinzi wa Rais Kabila, kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Ikulu ya nchi hiyo.
Mwandishi wetu Lubunga Bya'Ombe akiwa Kinshasa amethibitisha kumetokea taarifa hizo. Hata hivyo watu waliohusika bado hawajajulikana.
Taarifa zaidi tutawaletea kadri zitakavyokuwa zikipatikana.


IZ IT INDIAN GIRLS ARE COLD?

Inasemekana hivyo ila mimi sijawahi kupruvu hivyo,tungependa kupata maoni tokwa kwa wadau


 NYUMBA YATEKEKETEA MOTO MTONI KWA AZIZ ALLY HUSIKU WA JANA
Gari la zima moto likiwa katika eneo la tukio wakati ilipotokea ajari ya moto ambabpo chanzo chanzo cha moto kilianzia kwenye salon ya kiume.


No comments:

Post a Comment