Pages

Pages

Friday, February 4, 2011

     MISRI BADO HAPATOSHI,U.S.A YAINGILIA UTATA

Marekani imesema inafanya mashauriano na serikali ya Misri kuhusu utaratibu wa rais Hosni Mubarak kukabidhi madaraka.
Maandamano eneo la Tahrir
Maandamano eneo la Tahrir
Taarifa zinasema kuwa mojawapo wa masuala yanayozingatiwa ni Bw Mubarak kujiuzulu na kukabidhi mamlaka kwa baraza la kikatiba.
Serikali ya Marekani hata hivyo imesisitiza kuwa uamuzi kamili utatoka kwa watu wa Misri.
Wakati huo huo umati mkubwa wa watu umekusanyika kwenye eneo la wazi la Tahrir mjini Cairo wakishinikiza kuondoka mamlakani kwa rais Mubarak.
Ikilinganishwa na siku za awali, maandamano ya leo ni matulivu na waziri wa ulinzi Mohammad Hussein Tantawi ametembelea eneo hilo na kuwahutubia waandamanaji.
Kuna ulinzi mkali kwenye maandamano hayo huku wanajeshi wakishika doria.
Bw Mubarak alisema siku ya Alhamisi kuwa alihofia kutakuwa na machafuko iwapo ataondoka madarakani sasa.


TWANGA PEPETA YAFULIA,NANE WAKIMBILIA EXTRA BONGOKutoka kushoto ni muimbaji kiraka wa Twanga Charles Gabriel 'Charles Baba' , Hegga katikati na muimbaji Janet Isinika.
Kiongozi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki (katikati mbele), akiwa na wanamuziki wapya kutoka bendi ya African Stars 'Twanga Pepeta' wakati wa mkutano na waandishi wa habari alipokuwa akiwatambulisha wanamuziki hao kwa waandishi wa habari. Wanamuziki hao waliojiunga na bendi hiyo ni Mwimbaji Rogert Katapillar, Rapa wa bendi hiyo Saulo John 'Ferguson' ambaye aliibukia katika bendi hiyo hiyo ya Extra Bongo na Kiongozi wa Wanenguaji wa Twanga, Super Nyamwela, Danger Boy na Otilia. Pi


UKIJAMBA MALAWI IMEKULA KWAKO MJOMBA...!!!
Mzozo umezuka nchini Malawi kufuatia mapendekezo kutaka kufikishwa bungeni kuhusu kujamba, kuwa ni kosa.

Waziri wa sheria wa Malawi, George Chaponda amesema muswada huo utakaojadiliwa kuwa sheria ndani ya bunge wiki ijayo, utapiga marufuku kabisa kwa mtu kufanya haja hiyo hadharani. Waziri huyo amekiambia kituo kimoja cha radio nchini humo- kwa maneno yake - "nenda chooni kama unajisikia kujamba".


Hata hivyo mkuu wa wanasheria nchini Malawi Anthony Karanga amesema kufanya haja hiyo hakufikii kuharibu hali ya hewa kiasi cha kuwa kosa la jinai.

Mwandishi wa BBC nchini humo anasema wananchi wa Malawi wanajiuliza mapendekezo ya sheria hiyo, iwapo itapitishwa, itatekelezwaje?

 VIPI SHERIA HII IKJA BONGO...ITAFUNGA WENGI. HAA HAAA...!!

No comments:

Post a Comment