Pages

Pages

Thursday, April 28, 2011

MAJANGILI WA KISOMALI WAKAMATWA MOROGRORO



Kundi la Wasomali likiwa chini ya ulinzi kwenye kituo kikuu cha polisi mkoani Morogoro.
WATU wapatao 82 raia wa Somalia wamekamatwa jana mchana kwenye msitu wa moja ya vijiji vya Wilaya ya Gairo mkoani hapa wakiwa safarini kuelekea jijini Dar es salaam kutafuta maisha.

Akizungumza na mtandao huu kwenye kituo kikuu cha polisi mkoani hapa, askari mmoja wa kikosi cha kutuliza ghasia wilayani Gairo maarufu kwa jina la 'voda fasta'alisema Wasomali hao walikamatwa baada ya polisi kupokea taarifa kutoka kwa raia wema.

"Tumepokea taarifa kutoka kwa raia wema wakitujuza kuwa kuna kundi la wasomali wanakata mbuga katika misitu ya Vijiji vya Gairo hivyo baada ya kuwafuatilia tumewakamata na kuwaleta hapa mkoani," alisema afande huyo aliyekataa kutaja jina lake kwa kuwa sio msemaji mkuu wa jeshi la polisi.



MAWAKALA MISS TAZANIA KUPIGWA MSASA 




Semina ya Mawakala wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2011 itafanyika tarehe 29 na 30 April 2011 katika hotel ya Paradise City iliyopo Posta jijini D’salaam.
Semina hii itahusisha Mawakala wote wa Mikoa, na Kanda wanaoandaa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania.
Katika semina hiyo ambayo pia itakuwa ni Mkutano wa mwaka wa Waandaaji wa Miss Tanzania katika ngazi za Mikoa na Kanda, mambo kadhaa yatazungumzwa ikiwemo, kukumbushana Kanuni, Sheria na Taratibu za Mashindano ya urembo ya Miss Tanzania, maadili na miiko ya uongozi, na uendeshaji wa mashindano.
Pia Changamoto mbalimbali zinazokabili mashindano ya urembo zitajadiliwa.
Mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu kutoka katika Fani ya urembo na Taasisi mbalimbali. Orodha ya Mawakala imeambatanishwa.



Barcelona 2 Real Madrid 0

Nyota wa Barcelona Lionel Messi alifunga mabao mawili ya haraka haraka katika dakika za mwisho, na kuipa nafasi kubwa Barca kucheza fainali ya Klabu Bingwa Ulaya.
Messi
Messi
Kulikuwa na mvutano mkali kati ya timu hizo mbili, katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali, hadi pale Pepe wa Real alipopewa kadi nyekundu katika dakika ya 61.
Baada ya kadi hiyo, Barca walianza kutawala, na kupata magoli hayo mawili.


PILI HASHIM NDIO MISS TANGA CITY CENTRAL 2011


Hatimae mnyange wa kitongoji cha Miss Tanga City Central amepatikana huku shindano hilo likiacha historia kubwa. Mwanadada Pili Hashim ndie aliyabahatika kuvaa taji hilo ambalo hapo kabla lilikuwa likishikiliwa na Anna Kiwambo mrembo wa kitongoji hicho kwa mwaka jana. Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mishi Juma huku nafasi ya tatu ikienda kwa Salha Ibrahim. Kitongoji ca Miss Tanga City Central kiliandaliwa na kampuni ya Green Apple Entertainment kwa udhamini mkubwa wa Madam Hair Dressing Saloon, Mwanakodo, Sarah Issa, Arbab MB pamoja na Anko Mo Blogspot. Warembo wanne wamebahatika kuingia kunako kambi ya Miss Tanga 2011 ambapo kwa mwaka huu inaandaliwa na kampuni ya New Face Entertainment na itafanyika tarehe 11/06/2011 pale Mkonge Hotel. Kabla ya hapo Miss Tanga ilikuwa ikiandaliwa na kampuni ya Five Brothers Entertainment.

Pili Hashim na Mishi Juma ndio walibahatika kuingia fainali. Na hapa ilikuwa presha inapanda, presha inashuka mpaka alipotangazwa mshindi.

Top Five ya Miss Tanga City Central 2011....Pili Hashim (4), Rukia Shemdoe (1), Salha Ibrahim (3), Judith Kitogo (2) na Mishi Juma mwenye namba (5).....

Anaitwa Anna Kiwambo, ndie aliyekuwa anarudisha taji baada ya muda wake kumalizika. Anna Kiwambo pia ndie Miss Tanga 2010.

Kundi la Town Boys wakitoa burudani

Majaji wakiwa makini wakifuatilia warembo.

Warembo wa Miss Central wakipita na vazi la ufukweni.

Wakifungua show......


Mwana mfalme na Kate kufunga ndoa

Mwana mfalme William na mpenzi wake Kate Middleton

Ndoa ya kifalme inayofanyika leo nchini Uingrezea inafuatiliwa kwa makini nchini Ujerumani vile vile. Jumuiya moja ya hapa nchini inayoifuatilia ndoa hiyo kwa moyo wote inataka ufalme urudishwe

Mwenyekiti  wa  chama jumuiya hiyo  inataka kurudishwa a kwa mfumo wa kifalme  nchini Ujerumani Knut Wissenbacha  amesema, ''Sisi   katika  chama  chetu  kinachoitwa  Jadi  na Maisha  tumejipa jkumu   la  kuunga   mkono  wazo  juu ya kurudishwa  tena mfumo wa  kifalme  nchini  Ujerumani  na  kuudumisha"
Mwenyekiti  huyo, Bwana  Wissenbach haishi  katika kasri  bali nyumba ya kawaida  katika mji  wa  Niederheimbach ulioko jimbo la kaskazini  mwa Ujerumani.  Mpenda ufalme huyo ambaye  sasa ana umri wa miaka 40 ni mtumishi wa serikali.  Anapitisha  wakati wake wa faragha kwa kukusanya picha za wafalme wa kijerumani, nishani na sare za  wafalme.  
Katika ofisi  yake ameweka  tandiko  la  farasi  badala  ya  kiti.
Maharusi: Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa pili na mpenzi wake Kate MiddletonBildunterschrift: Maharusi: Mjukuu wa Malkia Elizabeth wa pili na mpenzi wake Kate Middleton


Rihanna Shows Off Her Legs & Gets Celebrities

Look at that girl with them daisy dukes on! Rihanna was spotted leaving Phillippe Chow in West Hollywood yesterday in her short shorts and Christian Louboutin Mary Jane pumps.  Later that day, she was seen getting a full body scan at LAX airport  before heading off to New York City.




This Is Why Shaq And Hoopz Need Their Own Reality Show

Former Flavor of Love winner Hoopz and her current boyfriend Shaquille O’Neal left Boston reporters in amazement as they worked out together during an upcoming segment on WCVB in Boston. A few months ago, The Boston Globe reported that Hoopz is filming a reality show based on her suburban life and her desire to become a women’s health and self-defense guru. Shaq, who currently lives in the same house, will be a part of the show.


No comments:

Post a Comment