Pages

Pages

Sunday, April 24, 2011

bREAKING NEEWS ...KONDA WA DALADALA NAE ATOA TIBA YA KIKOMBE..!!




MKAZI wa Mbagala jijini Dar es Salaam, ameibuka na kusema kuwa ameoteshwa na Mungu kutoa dawa kwa njia ya kikombe kutibia wagonjwa wenye maradhi sugu.
Dawa hiyo amedai Mungu amemuotesha kutoa dawa ambayo ni maji ya kisima, bomba na haichanganywi na chochote zaidi ya maji hayo.

Awali kijana huyo aliyekuwa akiabudu dini ya Ukristo na baadae kubadili dini na kuwa Muislam na ndipo ameoteshwa.

Awali imedaiwa kijana huyo alikuwa akifanya kazi ya ukonda katika daladala na hivi karibuni ameibuka na kudai kuwa ameoteshwa.

Kufuatia taarifa hiyo watu wameanza kujitokeza nyumbani kwa kijana huyo kupata kikombe cha dawa hiyo huku akiwa ameshika msaahafu mkononi.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi Temeke, wanafanya jitihada za kufanya mahojiano maalum na kijana huyo na taarifa itatolewa kwenye vyombo vya habari.

Kijana huyu ni wa saba kujitokeza na kudai wameoteshwa na Mungu na wengine wamejitokeza katika mkoa wa Mbeya, Moshi, Mbeya, Iringa, Tabora na Morogoro, Pwani wote wakidai kuoteshwa na Mungu kutoa tiba kwa njia ya kikombe.



NGUMI KUPIGWA PANANDIPANANDI ILALA BUNGONI 


     MABONDIA wa ngumi za ridhaa wa mkoa wa Ilala wanatarajia kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa Panandipanandi, Ilala Dar es Salaam. ambapo kutakuwa na ngumi kutoka kwa mabondia mbalimbali toka pande zote za mkoa wa DAr es Salaam

     Tamasha hilo litakalokuwa likitimua vumbi kila wiki inatarajia kuwakutanisha mabondia wa Ilala na wa sehemu nyingine za Dar es Salaam ili kuweza kujipima nguvu katika kuinua mchezo huo katika mkoa huo.

       Katika Tamasha hilo kesho bondia Mbwana Matumla anayejiaandaa kwa ajili ya kushiriki katika kuwania ubingwa wa UBO pambano linalotarajia kufanyika siku ya Mei mosi katika ukumbi wa PTA dhidi ya Mkenya Gabriel Ochieng atachuana na mabonmdia Yohana Robert na Issa Sewa.

      Akizungumza Dar es Salaam leo, Mratibu wa Tamasha hilo kup itia Taasisi ya Kinyogoli foundation, Habibu Kinyogoli alisema mapambano yote yatakuwa katika raundi nne huku pambano la Mbwana likiwa katika uzito wa Kg 55 likiwa ni sehemu ya maandalizi ya pambano lake hilo.

     Alisema, mkakati huo wa kuanzisha Tamasha akishirikiana na kocha msaidizi wa timu ya mkoa huo Rajabu Mhamila 'Super D' utasaidia kuinua vipaji vipya vya mchezo huo kwa kiasi kikubwa kwani kutawajenga wachezaji kujikita katika mchezo huo na kuufanya kama ndio ajira yao.

   Alisema, katika kulifanikisha hilo anawaomba wadau mbalimbali kuwasaidia kuwadhamini ili waweze kufikia malengo yao katika kuinua vipaji hivyo.pia alisema kutakuwa na wageni waalikwa ambao watatoa mada mbalimbali kuhusu kuinua mchezo wa ngumi Tanzania akiwemo mdau wa ngumi.Innocente Melleck na mwingine Benedictor Hulilo ambao watakuwa wageni waalikwa.


 MAKAZI YA GADDAFI YABOMOLEWA
Waasi Mjini Misrata
  Mapigano makali yanaendelea mjini Misrata licha ya serikali kutangaza kusitisha mashambulio dhidi ya waasi
  Ndege za kijeshi za shirika la Nato zimeangusha makombra kwenye mkaazi ya Kanali    Muammar Gaddafi mjini Tripoli.
  Walioshuhudia wanasema makombora hayo yamesababisha uharibifu mkubwa kwenye eneo Bab al Azizia.
Waasi wakikatisha katika mitaa ya mji wa Misrata

  Milipuko hiyo inasemekana kuwa mikubwa zaidi kusikika mjini Tripoli na ilisababisha vituo viwili vya kitaifa vya televesheni kukatiza matangazo yao kwa muda wa nusu saa.
  Matangazo ya vituo hivyo Jamahiriya na Shababiya yalikatizwa muda mfupi baada ya saa sita usiku baada ya shambulio hilo la Nato mjini Tripoli.
  Majeshi ya Nato yamekuwa yakishambulia majeshi na kambi za jeshi za Kanali Gaddafi baada ya kuidhinishwa na baraza la usalama la   Umoja wa Mataifa. Nia ikiwa kuwalinda raia wa   Libya waliokuwa wakilengwa na majeshi.
Awali, Kiongozi wa Upinzani, Mustafa Abdel  Jalil amesema Kuwait imekubali kuwapa dola milioni 180 kama msaada, huku wakiendelea na mikakati ya kupambana na majeshi ya serikali ya kanali Gaddafi.
  Bw Jalili ambaye pia ni Mkuu wa baraza la kitaifa la serikali ya mpito nchini Libya, amesema wanahitaji msaada huo wa kifedha kwa wakati huu.
  Kwengineko mapigano makali zaidi yameendelea mjini Misrata licha ya serikali kutangaza kuwa inasitisha mapigano.
Lakini msemaji wa serikali Moussa Ibrahim amesema jeshi linajibu mashambulizi kutoka kwa waasi.



             POMBE SI CHAI MNENGUAJI AKUDO IMPACT AZIMIKA
  Katika nderemo za Pasaka, ndani ya Ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Dar, mrembo mpya wa Bendi ya Akudo Impact ‘Vijana wa Masauti’ katika safu ya unenguaji, Mariam Sagwa alijikuta akidondoka stejini na kuzimika kwa dakika kadhaa baada ya kupandwa na ‘mzungu’ wakati akinengua.


Hata hivyo, wanenguaji wenzake walimpiga ‘tafu’ ya kusimama lakini alionekana akiyumbayumba hadi alipotolewa stejini.





  WATOTO WABAKWA UBUNGO
         Uchunguzi wa blogu hii umebaini kuwa idadi kubwa ya watoto ombaomba wenye umri kati ya miaka minne mpaka kumi hubakwa na vijana wenye umri mkubwa zaidi kutokana na mazingira hatarishi wanayoishi ya kulala nje huku wakisumbuliwa na mbu,mvua,baridi na kubakwa hasa kwa wato wa kiume hulawitiwa .
         Duru za habari zinamuomba rais Jakaya kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali kuwanusuru watoto hao kwani wanaathirika kisaikorojia na kupoteza imani na malengo ya maisha ya baadae,pia ni kinyume na haki za binadamu kwa mtoto kuingiliwa kinyume na maumbile.
                 Vitendo hivi hufanyika kwa watoto waliopo maeneo ya ubungo tanesco,inauma sana jamani...!!


Mabomu yalipuka Nigeria


Milipuko ya mabomu Nigeria
      Mabomu matatu yamelipuka mjini Maiduguri kaskazini-mashariki mwa Nigeria, na kuua takriban watu watatu.
      Mabomu mawili yalilipuka kwenye hoteli na jengine kwenye kituo cha usafirishaji siku ya Jumapili usiku.
Polisi wamesema walioathirika wamepelekwa kwenye hospitali mbili tofauti mjini humo.
      Kundi la kiislamu la Boko Haram linalopinga vitabu vya magharibi limelaumiwa kwa mashambulio kama hayo ambalo limekuwa likipambana na majeshi ya usalama mjini hapo.
      Milipuko ya hivi karibuni imetokea kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa magavana siku ya Jumanne katika majimbo 36 ya Nigeria.
     Ghasia ziliibuka kaskazini mwa Nigeria kufuatia uchaguzi wa rais Aprili 16, ambapo Bw Goodluck Jonathan aliyetoka upande wa kusini aliibuka mshindi.
Mamia wanaaminiwa kuuawa na maelfu wamekimbia makazi yao.
     Haikufahamika iwapo milipuko hiyo ya mabomu mjini Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, lina uhusiano wowote na ghasia hizo.




MISS KILIMANJARO YAANZA KULINDIMA..!!     Baadhi ya Warembo watakaowania taji la miss Kilimanjaro wakiwa katika pozi, Dar es salaam jana kabla ya kwenda kuweka kambi rasmi itakayoanza mwanzoni mwa mwezi ujao mkoani Kilimanjaro. kutoka kushoto ni Catherine Edwin,Diana Lymo na Jackline John

Catherine Edwin
Jackline John
Diana Lymo
Miss kilimnaro iedhaminiwa na Vodacom,Redds,Bamm solution,kilimanjaro bus service,kilimanjaro safari lodge,Africa sana pub,Rafiki min super market,Snow view hotelRahisi petrol stationMoshi fm,Fortune MountainresortVia africa busness solutionBen Expetation,OrientalBureau de change,www.uniqueentertz.blogspot.com na Shear Ellusion.


Arsenal yabomotwa 2-1 na Bolton

Matumaini ya Arsenal kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England yamefifia zaidi baada ya kufungwa 2-1 na Bolton.
Bolton
Bolton
   Arsenal wakicheza chini ya kiwango chao katika kipindi cha kwanza walifungwa na Daniel Sturridge kwa bao la kichwa kufuatia mpira wa kona.
   Mapema katika kipindi cha pili, Kipa Wojciech Szczesny aliokoa mkwaju wa penati uliopigwa na Kevin Davies, na dakika moja baadaye Robin Van Persie kufunga bao la kusawazisha kwa Arsenal.
  Arsenal walikuwa na nafasi za kutosha kushinda mchezo huo, lakini walijikuta wakipoteza katika dakika ya mwisho.
Tamir Cohen aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona na kuwapa ushindi Bolton.
  Arsenal walitakiwa kupata ushindi katika mchezo huu ili kuwa na matumaini ya kuwania ubingwa.



Watu 57 wameuwawa mapigano Sudan Kusini

     Katika vita baina ya jeshi la serikali na wapiganaji wakati Sudan Kusini inapojitahidi kupambana na uasi katika eneo hilo.
Raia wa Sudan Kusini
Raia wa Sudan Kusini
               Serikali ya Sudan Kusini inajitahidi kupambana na uasi wakati nchi hiyo inajitayarisha kujitenga na Sudan Kaskazini, ambapo uhuru unatarajiwa mwezi wa Julai.
Mapigano yalizuka baina ya jeshi la Sudan Kusini na wapiganaji wake wa zamani waliokuwa wakisubiri kujumuishwa kwenye jeshi la jimbo lenye mzozo la Jonglei.
               Zaidi ya wapiganaji 55 waliuwawa na wanajeshi na raia 70 walijeruhiwa.
Idadi hiyo huenda ikaongezeka, maelezo yakitolewa.
               Sudan kusini inajaribu kuzima uasi wa vikundi kama saba vya waasi, huku inakaribia uhuru kamili katika miezi mitatu ijayo.
               Umoja wa Mataifa unasema watu zaidi ya mia nane wameuwawa na 94,000 wamelazimika kuhama makaazi yao tangu Januari.
               Mzozo huo unatia wasiwasi kuhusu mustakbali wa taifa hilo jipya.
Katika siku za karibuni, watu wamehamishwa kutoka jimbo muhimu la mafuta la Unity, baada ya mapigano ya siku nne.
               Sudan Kusini imeishutumu serikali ya Sudan Kaskazini, kwa kuwasaidia wapiganaji wa kusini, madai ambayo yamekanushwa na kaskazini.


Dirty Money’s Dawn & Kaleena Sing The National Anthem For Knicks vs Celtics Game 3


       Dirty Money’s Dawn Richard & Kaleena hit up Madison Square Garden before their NY tour stop last night, to sing the National Anthem for the Knicks vs Celtics Game. The Celtics went on to beat the Knicks 113-96, placing them at a game away from shutting the Knicks out of the Eastern Conference playoffs.



  UJASILIAMALI WA WIKI

Mjasilia mali akiwajibika kutafuta ridhiki ya siku



Naomi Campbell to tie the Knot

 CampbellVlad
      After being embroiled in a blood diamond scandal, and cases of assault on her employees, Naomi Campbell is making headlines for a happier reason.Wedding bells are set to toll in what's going to possibly be the wedding of the year on December 7 & 8, 2010.
Naomi and her long time boyfriend Vladimir Doronin have set the date for the ceremony, which will take place in Egypt's grand Luxor Temple.The bride and groom reportedly will spend their honeymoon in Luxor at the Winter Palace Hotel. 
    Their bridesmaid will be their long time friend Dasha Zhukova, an entreprenuer and designer.
    Meanwhile, Vladimir Doronin is said to be still married to his wife Ekaterina, who he has been with for 21 years, and has a daughter with him. Vladimir is said to be Russia's version of Donald Trump.


TAIFA STARS YATUNDIKWA 2-0 NA MSUMBIJI







MABAO mawili ya mshambuliaji Jeremias Sitoe katika kila kipindi yameipatia   Msumbiji (Mambas) ushindi wa 2-0 dhidi ya Tanzania (Taifa Stars) kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku (Aprili 23 mwaka huu) 


     Mechi hiyo maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja huo wa kisasa uliojengwa na Wachina na wenye uwezo wa kuchukua watazamaji ilikuwa ya ushindani wa hali ya juu.


     Rais Armando Guebuza wa Msumbiji ndiye aliyezindua uwanja huo.Sitoe alifunga mabao hayo dakika ya 19 na 51 karibu kwa staili ileile baada ya mabeki wa kati Aggrey Morris na Nadir Haroub 'Cannavaro' kujichanganya katika kucheza mipira mirefu aliyopigiwa mshambuliaji huyo mwenye kasi na pia kudhani ameotea.

No comments:

Post a Comment