Pages

Pages

Monday, April 11, 2011

MUHINDI AMCHOMA MOTO MTANZANIA KWENYE ARDHI YAKE

           kijana wa kitanzania aliechomwa moto na muhindi huyo
    MTU  mmoja mwenye asil ya Kiasia anayehusishwa kumiliki hoteli moja maarufu iliyopo Kigamboni anadaiwa kumjeruhi kwa kumchoma moto mkazi wa Mjimwema, Lila Hussein (25), baada kuingia hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
          Akizungumza na Dar jana, ndugu wa majeruhi huyo, Abdullah Saiwaad,alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi majira kati ya saa 5:00 na 6:00 usiku.
           Alisema kabla ya kuchomwa moto, Lila ambaye amelazwa wodi namba 7 katika Hospitali ya Temeke akiwa hajitambui, alivuliwa nguo kisha kumwagiwa mafuta ya petroli na kwamba amejeruhiwa vibaya kuanzia sehemu za magotini hadi shingoni.
Alisema chanzo cha tukio hilo ni Lila kuingia kwenye muziki hotelini hapo bila kulipa kiingilio.
          “Hali ni tete, Lila yupo hospitali ya Temeke akipigania maisha yake baada ya kuchomwa moto na mhindi ambaye ni mmiliki wa hoteli ya South Beach, ameungua vibaya tunamwomba Mungu anusuru maisha yake,” alisema Saiwaad.
           Alisema baadaye aliokolewa na wafanyakazi wawili baada ya kuamua kupeleka taarifa kijijini Mjimwema.
           Kutokana na tukio hilo wanakijiji wametishia kuchoma moto hoteli hiyo na kwamba hali hiyo imesababisha mkuu wa kituo cha Kigamboni kupeleka askari wa doria kusimamia usalama hotelini hapo.
  Hapa ndipo tunapokumbuka sera za mchungaji mtikira....



JUSTIN BIEBER AFANYA MAZOEZI NA FC BARCELONA!


Dogo Star wa Pop,Justin Bieber toka Canada alichukua muda wake wa kupiga Tour yake iitwayo My World Tour nchini Spain kwa kufanya mazoezi ya soka na kikosi cha FC Barcelona toka Catalan pande za Joan Gamper Sports Complex,Barcelona Justin Bieber anayetumia mguu wa kushoto,alialikwa kufanya mazoezi baada ya kuoneka amevaa jezi ya FC Barcelona alipokua anacheza soka na crew yake na baadaye kufunguka kuwa yeye ni mpenzi mkubwa wa FC Barcelona,baadaye kuendelea na tour yake jijini Madrid!
JUSTIN BIEBER AKIWA NA BOJAN KRKIC


Atumia Tsh. Milioni 50 Kwaajili ya Harusi ya Mbwa Wake


Louise Harris akiwa na mbwa wake Lola na mbwa Mugly wakati wa sherehe ya Harusi
Monday, April 11, 2011 12:30 AM
Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ametumia paundi 20,000 (Karibia Tsh. Milioni 50) kwaajili ya kuandaa harusi ya kifahari na gauni la harusi la kifahari kwaajili ya mbwa wake wa kike.
Louise Harris mwenye umri wa miaka 32 alitumbua paundi 20,000 kwaajili ya harusi ya kifahari ya mbwa wake wa kike anayeitwa Lola ambaye aliozeshwa kwa mbwa anayeshikilia taji la mbwa mwenye sura mbaya kuliko wote Uingereza anayejulikana kwa jina la Mugly.

Sherehe hiyo ya kifahari ilihudhuriwa na watu 80 ambapo gharama za kuukodisha ukumbi kwaajili ya harusi hiyo ya aina yake ilikuwa paundi 2,500.

Mbwa Lola alivalishwa gauni la harusi lenye thamani ya paundi 1,000 ambalo lilitengenezwa maalumu kwaajili yake na duka la vito vya thamani la Swarovski.

Mbwa Lola pia alivalishwa cheni shingoni na kikuku mguuni ambavyo vyote viligharimu paundi 750.

Maua ya kupamba ukumbi wa harusi yaligharimu paundi 1,000 wakati wapambaji wa ukumbi walilipwa kitita cha paundi 3,000.

Miongoni mwa gharama za harusi hiyo ni mabaunsa waliokuwa wakilinda usalama kwenye harusi hiyo ambao walilipwa paundi 400, madansa na wacheza shoo waliolipwa paundi 500, gari la kukodisha aina ya Bentley kwaajili ya maharusi liligharimu paundi 500 wakati Dj alilipwa paundi 500.

"Mbwa wangu ni fahari yangu na furaha yangu ni kuwafanyia kila kilicho kizuri", alisema bi Harris.

Bi Harris alisema kuwa furaha yake imetimia kwa kuona Lola amefanikiwa kupata mwenza wake wa maisha ambaye amekuwa akicheza naye wakati wote.




watoto wazuri wakipata kilauli na mziki lain


  mambo ya mwanza hayo weekend hii ni bata tuuuuuuu.....


BABU WA LOLIONDO KUBOFYABOFYA SIMU USIKU KUCHA

Mchungaji Mstaafu Ambilikile Mwasapile akipokea zawadi ya simu kutoka
iliyotolewa na Kampuni ya Simu ya Mkononi Airtel,anayemkabidhi ni Meneja wa Biashara wa Airtel Mkoa wa Arusha ,Pascal Bikomagu kulia ni DC wa Wilaya ya Ngorongoro Elias akishuhudia tukio hilo

No comments:

Post a Comment