Pages

Pages

Tuesday, April 12, 2011

CCM WASHANGILIA KUONDOKA KWA MAKAMBA WATU WAPOMBEKA ILE MBAYA

 
Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM wakipiga kura kuchagua wajumbe wa kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma jana jioni.
 
           CCM Makao Makuu Dodoma wamejipongeza kwa kula na kunywa kwa kile wanachosema ni kufurahia kuondolewa ofisini kwa
aliyekuwa Katibu Mkuu, Bw. Yusufu Makamba jambo walilokuwa wanalisubiria kwa muda mrefu.
           Baadhi ya wafanyakazi hao waliokutwa na Majira katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini Dodoma wakizungumza bila kutaka majina yao yaandikwe gazetini, walisema kwamba furaha yao hiyo imenogeshwa zaidi na kuondolewa kwa sekretarieti nzima ambayo ilikuwa mzigo mkubwa, sio kwa chama tu bali pia kwa watumishi wa chama.
             Walisema uwajibikaji wa watumishi ulipungua kutokana na maamuzi binafsi ya Bw. Makamba ambayo kila mara yalitolewa bila kuzingatia taratibu za utumishi na ajira. Kwamba baadhi ya watumishi walihamishwa kibabe kwa amri yake kwa sababu binafsi.
             "Kuondoka kwa uongozi wa Makamba kwetu ni sawa na kuzaliwa upya, ndio maana tuko hapa tukiburudika kwa furaha na kupongezana. Kuondoka kwao haikuwa kazi ndogo kwani tayari baadhi ya wajumbe walishapewa kiasi kikubwa cha pesa ili kukwamisha na kuhujumu uamuzi wa kuwaondoa madarakani," alisema mmoja wa wafanyakazi hao.
             Mwingine alisema, "Ni kweli chama kimepoteza mvuto kwa wananchi kiasi kwamba hata sisi watumishi tunapata shida na aibu kila tunapoumbuliwa na kukejeliwa na wananchi mitaani. Hatuna la kusema wananchi wanapokilalamikia chama, lakini viongozi kwa sababu za uswahiba wao usio na kikomo wanakauka au kutoa matamko ya ajabu dhidi ya wanachama na wananchi kwa ujumla.
 
 

OUATARA AOMBA HALI YA UTLIVU IWEPO IVORY COAST
Alassane Ouattara
           Rais wa Ivory Coast anayetambulika na jamii ya kimataifa, Alassane Ouattara, ametoa wito wa kuwepo kwa hali ya utulivu baada ya kumkamata mpinzani wake Laurent Gbagbo.
           Akitangaza kuanza kwa uchunguzi juu ya Bwana Gbagbo,alimuahidi kuwa atapata haki zake na kwamba tume ya haki na maridhiano itaanzishwa.
           Bwana Gbagbo alijisalimisha baada ya mashambulio ya kijeshi katika nyumba yake mjini Abidjan.
Alichochea mapigano hayo kwa kukataa kuondoka madarakani,huku akisisitiza kuwa ameshinda uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba mwaka uliopita.
             Lakini majeshi yanayomuunga mkono Ouattara yakavamia makaazi yake siku ya Jumatatu, huku vifaru vya Ufaransa vinavyosaidia vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vikiwa karibu.
             Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameridhishwa na hatua ya kukamatwa kwa Bwana Gbagbo,akisema hatua hio imemaliza mapigano ambayo hayakuwa na msingi,na kwamba umoja wa mataifa utaunga mkono serikali mpya.
            Rais wa Marekani Barack Obama pia aliridhishwa na kukamatwa kwake, na kutoa wito kwa makundi yenye silaha nchini Ivory Coast kuzisalimisha ili kutoa fursa ya kujenga mfumo wa demokrasia.


VIPAJI VYA NGUMI KUSAKWA DAR

Bondia Mohamed Matumla (kulia) akimrushia ngumi Fredy Sayuni wakati wa mpambano wa kujipima nguvu uliofanyika Amana CCM juz
Bondia Mbwana Matumla (kulia) akipambana na Yohana Robart wakati wa mazoezi ya kujipima nguvu yaliyofanyika katika ukumbi wa Amana


JUSTIN BEIBER AMWAGANA NA SELENA GOMEZ
    Habari za nyuma ya uzio zinasma kuwa justn ameachana na girlfriend wake selena kutokana tukio la hivi karibuni ambapo jutsin ameonekana akiwa katika hali ya kimahaba na kidosho mwingine hivyo selena akasitisha mahusiano hayo.


Kufungwa Man City, Mancini abeba lawama

Meneja wa Manchester City Roberto Mancini amebeba lawama kutokana na timu yake kuchakazwa mabao 3-0 na Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Roberto Mancini
Roberto Mancini
             Mabao mawili ya Andy Carroll yaliidhoofisha Manchester City wakidemadema kupata nafasi nne za juu za kucheza Ligi ya Ubingwa wa Ulaya, wakishikilia nafasi ya nne, pointi tatu mbele ya Tottenham ambao wana mchezo mmoja mkononi.
"               Hatukucheza vizuri dakika 20 za mwanzo wakati Liverpool walicheza vizuri, lakini usiku huu nilifanya makosa. Ni makosa yangu. Tungeweza kufanya vizuri," Alisema Mancini.
             Alifanya mabadiliko ya wachezaji watatu waliocheza katika mechi waliyoifunga Sunderland mabao 5-0 wiki iliyopita.
              Bado Manchester City wanakibarua kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa siku ya Jumamosi wa nusu fainali Kombe la FA dhidi ya mahasimu wao wakuu Manchester United katika uwanja wa Wembley.
              Zaidi ya kuwa na usiku mbaya, Manchester City imepata pigo jingine baada ya mshambuliaji wao wa kutumainiwa Carlos Tevez kuumia misuli ya paja, ikiwa na maana huenda mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentine huenda asicheze mechi dhidi ya Manchester United.
             Bila ya kuzama kwa kina juu ya makosa anayosema ameyafanya, Mancini ameongeza: "Ninawaomba radhi mashabiki. Hata mimi mwenyewe nimefedheheshwa. Nimefanya makosa kwa mchezo huu na sio kwa wachezaji, wachezaji walicheza kwa kiwango chao cha asilimia 100.
            "Nilifanya makosa katika siku mbili zilizopita, naelewa kwa nini. Ni muhimu kuelewa hili kwa ajili ya pambano lijalo. Ni makosa yangu kwa sababu hatukujiandaa vizuri."
           Mshambuliaji Edin Dzeko, ambaye hajafunga katika mchezo wa ligi tangu alipojiunga na Manchester City akitokea Wolfsburg mwezi wa Januari, alichukua nafasi ya Mario Balotelli, ambaye awali aliingia badala ya Tevez, na kiungo Gareth Barry pamoja na James Milner waliingia badala ya Nigel de Jong na David Silva.
"Nilifanya mabadiliko ya wachezaji watatu, nikaingiza wachezaji watatu wapya, mtazamo wetu haukuwa sahihi," aliongeza Mancini. "Liverpool walicheza vizuri sana katika dakika 20 za mwanzo,            tuliwaachia wacheze wanavyotaka, na walikuwa wakali mwanzoni na sisi tukawa tumepoa.


 KERY HILSON KIONEKANA KWENYE PICHA ZA UTUPU



    Kery Hilson alipigwa picha na Patrick Demarchelier,na amefunguka kuwa “tunafanya vitu vingi,na nina handbags za thamani na kila kitu ila shooting ya jarida hili ni kuvitupa hivyo vyote na kulipamba jarida”
             Allure Magazine ni jarida maarufu sana nchini Marekani ambalo linajihusisha na urembo kwa wanawake,na huchapishwa kila mwezi na lilianzishwa mwaka 1991 na Linda Wells 

 

RACHEL UCHITEL AJIA NA NJEMBA MPYA UFUKWENI
       Tiger Woods isn't the only one back in the swing of things ... so is mistress numero uno Rachel Uchitel ... who busted out her tiny bikini and her new man for a beach day in Miami yesterday. 
Rachel says her 25-year-old BF Matt Hahn is,  "The best thing that's happened to me in as long as I can remember."
     Apparently, she's having trouble remembering the time she got a $10 million check from Señor Woods.

No comments:

Post a Comment