Pages

Pages

Monday, June 27, 2011

breaking news..MUAMMAR GADDAFI KUKAMATWA KAMA KUKU..!!

Kanali Muammar Gaddafi
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita imetoa hati ya kukamatwa kwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi.
Mahakama imemtuhumu kwa uhalifu dhidi ya binadamu na kuamuru mashambulio kwa raia baada ya machafuko dhidi yake kuanza kati kati ya mwezi Februari.
Mahakama hiyo iliyopo the Hague pia imetoa hati ya kukamatwa kwa washirika wake wakuu Kanali Gaddafi- mtoto wake wa kiume Saif al-Islam na mkuu wa kijasusi Abdullah al-Sanussi.
Maelfu ya watu wanaaminiwa kufariki dunia kwenye ghasia hizo.
Hati hizo ziliombwa na mkuu wa mahakama hiyo ya ICC Luis Moreno-Ocampo mwezi Mei, aliyesema watu hao watatu walihusika na "mashambulio yaliyopangwa na yaliyosambaa" kwa raia.
Bw Moreno-Ocampo alisema mahakama hiyo ina ushahidi kuwa Kanali Gaddafi "aliamuru binafsi mashambulio kwa raia wa Libya wasio na silaha na alihusika kwa kukamatwa na kunyanyaswa kwa wapinzani wake wa kisiasa.
Serikali ya Libya hivi karibuni ilisema haitambui mahakama hiyo na tishio la hati hiyo haiwashughulishi.





 MISS PWANI APATIKANA
Vodacom Miss Pwani Winifrida Gracian katikati akiwa na mshindi wa pili Thuraiya Dabas(kushoto) na mshindi watatu Mariaclara Mathayo kwenye shindano hilo lililofanyika jana katika ukumbi wa TASUBA,Pwani Wilaya ya Bagamoyo.



 DENDA NJENJE..!1

Martin akila denda ukumbini




VIJIMAMBO NJIANI
Kwa ujumla hali ya barabara ya Bujonde haifai kabisa ni tabu tupu hapa tumekwama.



MISS MWANZA 2011
Vodacom Miss Mwanza 2011 Irene Kalugaba akiwa a picha pamoja na =mshindi wa pili Vodacom Miss Mwanza Frola Razaro (kulia)a Monica James mshindi wa pili wa shindano la Vodacom Miss Mwanza lililofanyika kwenye hoteli mpya na ya kisasa kabisa ya Gold Crest karibu kabisa na hoteli kongwe ya New Mwanza Hoteli jijini Mwanza ambapo tayari shindano limekwisha na washindi ndioyo hao.
Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ziwa Bw Stephen Kingu akiwa katika picha ya pamoja na wafayakazi wenzake, kulia ni Janet Kambeson msaidizi wa Mkurugenzi wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Miriam Makalla Mwakilishi wa Mauzo Vodacom Kanda ya Ziwa , Bernald Kombe Activation Coordinator Lake Zone .
Hii ndiyo tano bora ya Vodacom Miss Mwanza kutoka kulia ni Ester Laurent, Monica James, Diana James, Irene Kalrgaba na Frola Razalo wakipozi kwa picha.
Majaji wa shindano hilo wakijadili jambo kabla ya kumtangza mshindi kutoka kushoto ni Cess Odemba Ben Mwangi,Cynthia Buhama
Kutoka kulia ni Rubeny , Msanii Mwasiti , Zamaradi Mketema wakibembeleza mtoto.
Lina wa THT na Sajna msanii kutoka mkoani mwanza.
Msanii Barnaba akipagawisha mashabiki wake wakati wa shindano la Vodacom Miss Mwanza lililofanyika katika hoteli ya Gold Crest Hotel.
.Vazi la Ufukweni kama unavyoona.
Hapa wakiendelea kupita na vazi la ufukweni.
Vazi la Ufukweni bado linaendelea.
Wasanii wa mwanza wakifanya vitu vyao jukwaani wakati wa shindano .
Mdau Flora kulia wa Mwanza akiwa na rafiki yake
Vazi la ubunifu
Hili limebuniwa kwa majani mapana yaliyokolea rangi ya kijani.
Hili limebuniwa kwa kitenge na shanga.

No comments:

Post a Comment