Pages
▼
Pages
▼
Wednesday, June 22, 2011
CONSOLATA LUKOSI BALOZI WA REDDS ANAYETAMBA KWA UBORA 2010-2011
Balozi wa Redds 2010 Consolata Lukosi wakati wa mashindano ya miss Chang'ombe mwishoni mwa wiki iliyopita akiwa katika pozi na kamera yetu.
Balozi wa Redds 2010 Consolata Lukosi akiwa na Bahati Chando miss Ilala 2010 na Salma Mwakalukwa Miss Ilala II 2010 wakati wa mmashindano ya miss Chang'ombe mwishoni mwa wiki iliyopita
Balozi wa Redds 2010 Consolata Lukosi akiwa na Salma Mwakalukwa Miss Ilala II 2010 wakati wa mashindano ya miss Chang'ombe yaliyofanyika ttc chang"ombe jijini Dar es salaam.
MISS SINZA KUALAMBA LAKI SITA
MSHINDI wa taji la Miss Sinza 2011, anatarajiwa kuondoka na zawadi ya fedha
taslimu Sh 600,000 katika shindano litakalofanyika Ijumaa kwenye ukumbi wa
Vatican, uliopo Sinza, Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Hadees,
jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa shindano hilo, Titina Makutika, alisema
kuwa mshindi wa pili atazawadiwa Sh 400,000, wakati wa tatu ni Sh 300,000.
Alisema kuwa mshindi wa nne na wa tano, kila mmoja ataondoka na Sh 200,000,
wakati wa sita hadi 15, kila mmoja atapata kifuta jasho cha Sh 100,000.
Titina alisema kuwa shindano lao linatarajiwa kusindikizwa na burudani kutoka
kwa bendi ya muziki wa dansi ya Mapacha Watatu na wasanii kadhaa wa Bongo Fleva.
Alisema kuwa maandalizi ya shindano hayo, yanaendelea vizuri na kwamba shoo yao
inatarajiwa kuwa katika ubora wa hali ya juu.
“Kutokana na warembo tulionao, tuna imani taji la Miss Kinondoni 2011, litatua
Sinza, ikiwa ni pamoja na lile la Miss Tanzania.
Aliwataja warembo watakaopanda jukwaani siku hiyo kuwa ni Stellah Moris (20),
Husna Maulid (19), Hanifa Halfani (18), Naomi Jones (19), Joyce Raphael (18),
Asha Julius (18), Anna Gerald (20) na Mariam Almas.
Wengine ni Felista Philip (19), Pamela Gordian (19), Winnie Gerald (18), Grace
Revocatus (20), Hellen Masawe (18), Stellah Premsingh (20), Jacqueline Joachim
(19) na Evelyna Rwandala (20).
Shindano hilo limeandaliwa na kampuni ya Calapy Entertainment na kudhaminiwa na
Vodacom, Redd’s, Fabeck Fashion, Jambo Leo, Cloud’s FM
No comments:
Post a Comment