Pages

Pages

Thursday, June 9, 2011

EXCLUSIVE: DULLY SYKES KUJIACHIA NA WAREMBO WA MISS KILIMANJARO


Mwanamuziki dully sykes a.k.a misifa atawasha moto katika shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa kilimanjaro.
Shindano hilo litafanyika tarehe 18 june katika hoteli ya salsanero iliyoko mjini moshi.





CHRISTINE BAX
christine_bax_147
Akiwa katika pozi tofauti
christine_bax_179
MOJA YA MAMODO WA VIDEO WANAOFANYA VIZURI KATIKA VIDEO MBALIMBALI ZA MASTAA WA ABROAD



 VITUKO VYA WEEKEND..!!
Mnenguaji Bakari"mandela" akiwa anamwaga radhi ukumbini.
Mrembo akiwa anajimwayamwaya na muziki wakati shanga zikiwa zimeruka kiuno


WANAMIBIA WAFANYA KWELI NIGERIA

 Ogopa DJs toka Kenya ambayo ina tawi nchini Namibia, imepata tuzo kupitia artist walio chini yao toka Namibia waitwao Gal Level

Gal Level walipata tuzo 3 kwenye Namibian Annual Music Awards (NAMAs) za Best Album of the Year na Best Female Artist,na Gal Level wanatarajiwa kwenda jijini Nairobi kwa ajili ya tour coz artist Amani toka Kenya alikua Namibia na alipiga showz kadhaa na Gal Level na Gal Level watakwenda Nairobi,na Amani alipokua pande hizo aliingia studio kupiga collabo na Gal Level
Gal Level kwenye usiku wa tuzo hizo walipata fedha taslimu,gari mpya na almasi toka Namdeb Diamond Corporation Limited.




Ubakaji watumiwa kama silaha Libya

Kiongozi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) amesema kuwa kuna ushahidi kwamba kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, aliamuru kubakwa kwa mamia ya wanawake kama silaha ya kupambana na waasi nchini mwake.

Wanajeshi wakiuzingira mji wa Misrata
Luis Moreno-Ocampo alisema kuwa ubakaji ni mbinu mpya inayotumiwa na Kanali Gaddafi katika ugandamizaji.
Alisema kuna uwezekano mkubwa kuwa wanajeshi waaminifu kwa Kanali Gaddafi walipewa madawa kama vile Viagra ili kunoa uchu wao wa kuwabaka wanawake.
Hadi kufikia sasa Serikali ya Libya haijasema lo lote kuhusu madai hayo.

Kanali Gaddafi
Mwezi uliopita, Bwana Moreno-Ocampo aliomba majaji wa mahakama hiyo ya ICC kutoa amri ya kuwakamata Kanali Gaddafi, mwanawe Saif al-Islam, na kiongozi wa Ujasusi nchini humo Chifu Abdullah al-Sanussi.
Aliwalaumu kwa kutekeleza uhalifu mara mbili dhidi ya binadamu - mauaji na mateso. Alisema watu hao watatu ndio wanaopaswa kujitwika lawama zote za mashambulizi dhidi ya raia tangu mwanzo wa maasi dhidi ya Serikali yaliyoanza Februari, wakati kati ya watu 500 na 700 wanadaiwa kuuawa.

No comments:

Post a Comment