Pages

Pages

Monday, August 29, 2011

REDD'S YATOA ZAWADI EL-FITRI KWA AKINA MAMA WAZAZI HOSPITALI YA MWANANYAMALA

Jenifer kakolaki,mshiriki wa Miss tanzania akimbembeleza mtoto
 Warembo wakimsikiliza Mganga mkuu katika hospitali ya mwananyamala jijini Dar.
Mrembo akisaini kitabu cha wageni kwa niaba ya warembo wenzake.
 Miche ya sabuni na nepi kwaajili ya watoto wachanga waliozaliwa, zawadi hizo zilikabidhiwa hospitalini hapo na warembo kupitia kinywaji cha REDD'S.
Mrembo akionyesha upendo kwa mama na mtoto.
Salha Israel akimbeba mtoto mchanga kwa furaha wodini hapo.
Ni upendo wa hali ya juu sana kwa warembo wa Miss Tanzania kuonyesha ushirikiano na watu tofautitofauti katika jamii yetu,hii imekuwa ikiwezeshwa na Redd's kinywaji murua.
Mrembo toka Tanga akishangaa mtoto alietoka kuzaliwa kama dakika kumi zilizopita,mi kupita REDD'S utatambua haya.
Brand Manager wa REDD'S ,Victoria akiongea na waandishi wa habari nia ya kutoa zawadi hizi kwa wamama waliojifungua miche ya sabuni na nepi kwaajili ya watoto wao wachanga.
Miss tanzania Geneviev Mpangala akiongoza warembo hao ambao walikuwa katika picha ya pamoja na madaktari wa hospitali ya Mwananyamala jijiniDar.
Ziara ilisitishwa kwa picha hii,pongezi REDD'S kuwafikia akina mama waliojifungua kipindi hiki cha Idd.


MAAZIMISHO YA MIAKA 47 YA JESHI LA WANAMAJI
 Wanajeshi wakionyesha wananchi namna ya kujiokoa na boya.
 Jinsi ya kuokoa mtu aliezama katika maji mengi.
Tukio hili lilikuwa likifanyika maeeneo ya kivuko cha kigamboni ambapo wakazi na wavuka boti walipata elimu hii leo.



NAIBU SPIKA MH. JOB NDUGAI AONGELEA UVUMI AMBAO UMEZAGAA KUHUSU KUTOFAUTIANA NA SPIKA WAKE

Mh. Anna Makinda (Spika)
Mh. Job Ndugai (Naibu Spika)
     Taarifa ambayo imeibuka kuhusu Spika na Naibu Spika kutofautiana kuhusu maamuzi ya kuunda Kamati maalum ya kumchunguza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo si ya kweli.
     Mh. Job Ndugai ameyaongea haya katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM cha leo na amekana huo ni uvumi tu wa watu ambao wasiolitakia mema taifa letu na wasioutakia mema ushirikiano wao mzuri ambao wanao yeye na Mh. Spika Anna Makinda, na vile vile Mh. Ndugai alilielezea pia uvumi ambao watu wameuzusha kuhusu yeye kuonekana ana nguvu zaidi ya Spika Anna Makinda; Mh. Ndugai amekana hilo na kusema ni maneno tu yale yale! ambayo watu wasioutakia mema ushirikiano wao na kusema kwamba Mh. Spika Anna Makinda anamuamini sana na anamtuma katika shughuli nyingi tu ambazo ni muhimu lakini anaenda yeye Mh. Job Ndugai.     Clouds Fm walimuuliza maswali mawili matatu naye akayaongelea kwa ufasaha na kutaka wananchi waelewe hivyo anavyosema yeye, kuliko kusikiliza watu ambao wanazusha tu mambo ambayo sio mazuri.




AMBER ROSE NA WIZ KHALIFA WALIVYOTINGA MTV AWARDS

Wiz Khalifa and Amber Rose were the perfect couple on the Black Carpet at the 2011 MTV VMAs held at the Nokia Center in California.
Amber Rose told the world that the only thing she's looking forward to is her man Wiz Khalifa winning Best New Artist!


Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makala akimsikiliza Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kwa Mbunge wake juu ya kitendo cha kubomolewa choo chake na Mwekezaji Raia wa kigeni na kuzungusha uzio uliofikia  upenuni mwa makazi yake. Mbunge huyo alitembelea kitongoji hicho mwishoni mwa wiki kujionea hali halisi ya mgogoro wa ardhi uliopo kijijini hapo.
 Makala akiongozwa kuangalia uzio uliowekwa na muwekezaji huyo na kuzua mgogoro wa ardhi wa kugombea mipaka na wanakijiji. Kushoto ni walinzi wa mwekezaji huyo.

No comments:

Post a Comment