Pages

Pages

Thursday, November 24, 2011

JACQUE PENTEZEL ADUNGWA UJAUZITO NA TIMBULO

                                       Habari za kidaku toka kwa rafiki wa karibu Msanii Timbulo zinasema kuwa Jacque Mpenteze ashadungwa ujauzito na kijana huyo msanii wa bongo Flava anaekuja kwa kasi katika staili za kubana pua.
  Penzi la Jacque na Timbulo limefikia sehemu nzuri si kiasi cha kuishi pamtu wanyetishaji wa habari hizi wamesea Haque ana ujauzito mdogodogo ambao bado haujaanza kuonekana pengine baada ya miezi kadhaa itakuwa sio siri tena.
  Kuzihilisha hayo ni kweli Msanii huyo aliimbia Uniqueentertz kuwa nyimbo yake mpya "wa leo wa kesho" ni mahususi kwa Mpenzi wake Jaque ambae ndiye chaguo lake la moyo kiasi cha kupa kibend binti huyo.

KATIBU WA BUNGE AONGEA NA WAANDISHI WA HABARI.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashillilah ( kulia ) akiongea na Waandishi wa Habari( ambao hawapo pichani) kuhusu jinsi miswada mbalimbali ilivyopitishwa kwenye kikao cha tano cha Bunge mjini Dodoma hivi karibuni, kulia ni Mkurugenzi wa Habari,Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa Bw. Jossey Mwakasyuka.
Dkt. Thomas Kashillilah (katikati ) akiongea na Waandishi wa Habari kwenye Ukumbi wa Bunge mjini Dar es Salaam kama picha inavyonyesha kuhusu jinsi Miswada mbalimbali ilivyopitishwa kwenye kikao cha tano cha Bunge mjini Dodoma hivi karibuni


MIKATO MIPYA YA HARUSINI

 Hii ni maalumu kwa akina dada wa leo wenye kwenda na fashion kwa muda muaafaka.



Wanajeshi wakivunja maandamano
Maafisa wawili waandamizi katika utawala wa kijeshi nchini Misri wameomba radhi kufuatia mauaji ya waandamanaji yanayoendelea katika mji mkuu Cairo na miji mingine nchini humo.

Majenerali hao wamejitokeza katika televisheni ya serikali wakitoa salaam za rambirambi kwa wananchi wa Misri.

Hii ni mara ya kwanza kwa watawala wa kijeshi kuomba radhi tangu mgogoro uanze nchini Misri.

Serikali itatangaza leo namna wanavyopanga kuendelea na shughuli za uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kuanza Jumatatu ijayo.

Ujumbe wa majenerali hao ulionekana kuwa wa kuwapa moyo watu kinyume na awali ambapo walionyesha ukali na tarayi kukabiliana na upinzani hususan kwenye hotuba ya kiongozi wa baraza tawala la jeshi Field Marshall Tantawi.



Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni Future Centery Helene Masanja,akizungumza na wahandishi wa habari kuhusu mechi ya kombaini ya timu za Simba na Yanga dhidi ya timu ya Kumasi Asante Kotoko ya Ghana,katikati ni Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Mwenyekiti wa DRFA Amin Bakharesa.

No comments:

Post a Comment