Pages

Pages

Sunday, November 6, 2011

PRINCE CHARLES KUPOKELEWA NA MABANGO YAKUPINGA USHOGA TANZANIA

                                      Baada ya Serikali kutoa msimamo wake juu ya masharti ya Serikali ya Uingereza kutoa misaada kwa nchi masikini ikiwamo Tanzania, ziara ya mtoto wa Malkia wa Uingereza, Elizabeth II, inatarajiwa kupokewa na mabango ya kupinga masharti hayo. 
  Prince Charles na mkewe Camilla, wanatarajiwa kuwasili nchini jioni ya leo kwa ziara ya siku tatu nchini, ambapo wanaharakati nchini wamepanga kumpa ujumbe wa kupinga masharti ya misaada kwa kulinda haki za mashoga nchini.
  Waandamanaji wenye mabango kwa mujibu wa habari zilizopatikana jana Dar es Salaam, watajipanga katika maeneo atakamopita mgeni huyo, wakiwa na mabango yanayounga  mkono kauli ya Serikali kulaani tishio la Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, la kukata misaada kwa nchi ambazo hazitaruhusu ushoga.
 
 Kitendawili cha nani atavaa taji la Miss World 2011 kinataraji kuteguliwa leo wakati wa Fainali za mashindano hayo zitakapo fanyika katikaukumbi wa Earls Court ndani ya jiji la London Uingereza. 
 Tanzania katika mashindano hayo ya urembo ambayo ni makubwa Duniani inawakilishwa na Miss Tanzania 2011, Salha Izarael Kifai. Tyari mapema wiki hii Salha alifanikiwa kuingia katika 16 bora ya shindano dogo la Beauty with Purpose. Blogu hii ya Father Kidevu inaungana na watanzania wote popote pale ulimwenguni kumtakia kila la heri Salha katika mashindano hayo. Mungu Mbariki Salha, Mungu ibariki Tanzania.
  Miss World 2011, the 61st edition of the Miss World pageant is scheduled to take place at the Earls Court Two on November 6, 2011 in London. As part of the events, the contestants also traveled to Edinburgh, Scotland between October 23 and October 27.. Alexandria Mills of the United States will crown her successor at the end of the event. Although over 120 delegates were expected to compete, problems regarding the timely acquisition of visas prevented several candidates from participating, thus reducing the final number to 115.


No comments:

Post a Comment