Pages

Pages

Sunday, November 27, 2011

RADI YAUWA MWANACHUO DODOMA

     Charles Mfaume ambaye alifariki hapo jana Mara baada ya kupigwa na Radi iliyoambatana na Mvua iliyonyesha Usiku wa jana Chuoni. Marehemu Charles Mfaume alikua ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa shahada ya kwanza ya biashara na utawala wa rasilimali watu. (BCOM HRM)
     Mwili wa Marehemu Unatarijiwa kuwasili Chuo Hapa Kwaajili ya Maombi na Kuagwa tayari kwa kusafirishwa kuelekea kwao Dar es Salaam tayari kwa mazishi. Sala na Zoezi zima la Kuaga mwili wa marehemu kwa mara ya mwisho litafanyika muda si mrefu kwenye kiwanja cha mpira wa kikapu kilichopo katika kitivo cha sayansi ya jamii cha Chuo Kikuu Cha Dodoma leo na kusafirishwa leo
        Vilevile Radi hiyo imesababisha wanafunzi wawili kulazwa zahanati ya chuo kutokana na majeraha aliyopata mmoja wa wanafunzi aliyefahamika kwa jina la Peter ambapo aliungua Mguu na Shingoni na Mwanafunzi mwingine Wa Kike huyu amelazwa baada ya kupoteza fahamu kutokana na mshtuko wa jana. Huu ni Msiba Wa Pili ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ndani ya Wiki moja Ambapo alhamisi iliyopita Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili Wa Kitivo Cha elimu Yohana Raphael kupoteza Maisha Ghafla mara baada ya kuanguka na kusafirishwa kwao Kigoma kwa Mazishi.    


MABINGWA WATETEZI KOMBE LA TUSKER CHALLENGE 2010 KILIMANJARO BOYS WALALA 1-0 KWA RWANDA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwapungia mikoni mashabiki kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii,  Mara baada ya kuzindua rasmi michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 ambapo leo michuano hiyo imekutanisha timu za Tanzania Kilimanjaro Stars na Timu ya taifa ya Rwanda Amavubi,  mpira umekwisha na timu ya Rwanda imeifunga Kilimanjaro Stars  goli 1-0 , katika picha kulia  anayecheka ni Rais wa TFF na Shirikisho la Vyama vya michezo Afrika Mashariki na kati CACAFA Leodger Tenga.


NATO YAUWA PAKSTAN KWA SHAMBULIO LA NDEGE
 Waziri Mkuu wa Pakistan, Yousef Raza Gilani, ameelezea shambulio la ndege za NATO dhidi ya kituo cha ukaguzi cha Pakistan kuwa shambulio dhidi ya umoja na uhuru wa Pakistan.
Taarifa zinazohusiana
Asia
Wanajeshi 25 wa Pakistan waliuwawa katika shambulio hilo karibu na mpaka wa Afghanistan.
Bwana Gilani alisema Pakistan imeungana na haitoruhusu mtu yeyote kuishambulia.
Bwana Gilani alikuwa anakwenda Islamabad kwa mkutano wa dharura kuhusu ulinzi, kujadili tukio hilo.
Jeshi limesema lina haki ya kulipiza kisasi.
NATO inasema inachunguza tukio hilo kujua ukweli
.

No comments:

Post a Comment