Pages

Pages

Wednesday, November 16, 2011

SALHAI ISRAEL AREJEA JANA TOKA UK

Miss Tanzania 2011, Salha Izrael akipunga mkono mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana akitokea jijini London Uingereza alikoshiriki shindano la urembo la Dunia Novemba 6,2011.
 Warembo na wanafamilia wakipiga picha ya pamoja na Miss Tanzania 2011, Salha Izrael.
Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Izrael (katikati) akiwa na baadhi ya warembo walioshiriki shindano la Miss Tanzania 2011 waliofika kumpokea katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana akitokea jijini London Uingereza alikoshiriki shindano la urembo la Dunia Novemba 6,2011. Warembo hao toka kushoto ni Jenifa Kakolaki, Alexia Willam,Hussna Maulid na Hamisa Hussein.


MASHINDANO YA NGUMI YA KOVA CUP YAENDELEA

Bondia Sunday Elius akipambana na Abdallah Kasimu wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Kasimu alishinda kwa point
Bondia Mussa Mohamedi (kulia) kushoto akioneshana ufundi wa kutupa makonde na John Christian wakati wa mashindano ya Kova Cup Dar es salaam jana Mussa alishinda kwa point.

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AKUTANA NA MABALOZI WA SUDAN NA JAPAN NCHINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Sudan nchini Tanzania, Dkt. Yassir Mohamed Ali, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo leo Novemba 16, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi mpya wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kwa mazungumzo na kujitambulisha leo Novemba 16, 2011. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment