Pages

Pages

Monday, November 28, 2011

TWANGA PEPETA YAKONGA MIOYO MIAKA 50 YA UHURU LONDON


 African Stars Entertainment Tanzania (Aset) ambao wanajulikana kwa jina la  “Twanga Pepeta” walikuwa  kivutio cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru London juzi Jumamosi. 
Kikosi hiki cha watumbuizaji maarufu wa Kibongo kilikaribishwa na  Urban Pulse, Jestina George wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania mjini hapa.
Watanzania wa kila rika, nasaba na taaluma walifurika toka miji ya Leeds, Bristol, Birmingham, Northampton, Milton Keynes na vitongoji mbalimbali kufurahia vigongo vya bendi hili lenye makao makuu Mango, Kinondoni Dar es Salaam. 
Ukumbi wa Club 2000 Banqueting Suite ulioko nyuma ya uwanja maarufu wa Wembley ulishuhudia tafrija hiyo wakati viongozi rasmi wa serikali walipofungua tafrija wakicheza nyimbo maarufu za Kitanzania kama ule wa mwanamuziki Salum Abdallah (“Wanawake wa Tanzania” na “Tujenge Nchi Yetu”) marehemu alizoimba mara baada ya Uhuru mwaka 1961.



JASIRI HAACHI ASILI

Makamu wa Rais Mh. Bilal akiwa na Waziri Mkuu akimpa maelekezo kuhusu mila za makabila ya Mkoa wa Rukwa na vitu wanavyotumia vya makabila ya huko.

 

MVUA YAKATA MAWASILIANO YA BARABARA KATI YA ARUSHA NA KARATU

Mawe yakiwa yamezolewa na maji hadi kuingia sehemu ya barabarani.

Hali ndiyo hii mdau.


Wananchi pamoja na watalii wanaotumia barabara inayo unganisha arusha na karatu leo wamekwama baada ya mto kirurumo uliopo mto wa mbu kukata barabara na kujaza mawe njiani vilele kwa mujibu wa wananchi waeneo hilo inasemekana mtu mmoja amepoteza maisha mto huo umefurika baada ya mvua kubwa iliyo nyesha usiku wa kuamkia leo.
Mwili wa marehemu Samweli Julius ambaye alikuwa ni msaidizi wa mitambo ya kutengeza barabara, ukiwa umenasa juu ya mti. 

No comments:

Post a Comment