Pages

Pages

Friday, December 30, 2011

BREAKING NEWS: MTANGAZAJI MKONGWE JOHN NGAHYOMA AFARIKI DUNIA

 Marehemu John Ngahyoma akiwa kazini enzi za uhai wake.
Tumepata taarifa kwamba Mwandishi wa Habari mkongwe nchini ambaye alikuwa akifanya kazi na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), John Ngahyoma amefariki dunia leo asubuhi.
Msiba uko nyumbani kwa marehemu Tabata, karibu na nyumbani kwa Marehemu Danny Mwakiteleko. Mwenye taarifa zaidi atufahamishe.
Tunaitakia moyo wa subira na Mungu awafariji wanafamilia wa Ngahyoma katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMIN

No comments:

Post a Comment