Pages

Pages

Thursday, December 29, 2011

BREAKING NEWS: MTANGAZAJI WA TBC AFARIKI DUNIA

Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC – HALIMA MCHUKA amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI Jijini DSM alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa kiharusi.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC CLEMENT MSHANA, HALIMA MCHUKA alikimbizwa katika hospitali ya DAR GROUP na baadae katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI hapo jana baada ya kuanguka ghafla akiwa katika kituo chake cha kazi eneo la PUGU ROAD Jijini DSM.
MCHUKA alikuwa mtangazajii wa kwanza wa kike wa mpira AFRIKA MASHARIKI.

No comments:

Post a Comment