Pages

Pages

Sunday, December 25, 2011

JAHAZI MOLDEN TAARAB YATIMIZA MIAKA 5 NA KUZINDUA ALBAM YAKE YA MPENZI CHOCOLATE

Hassan Yahya Mwinyi Katibu Mkuu wa kundi la Taarab la Safari Malindi kulia akimpongeza Khamis Koha Mkurugenzi Msaidizi wa kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, baada ya kuzindua rasmi albam yao mpya ijulikanayo kama Mpenzi Chocolate na sherehe za miaka 5 ya kundi hilo zilizofanyika mkesha wa Krismasi usiku wa kuamkia leo, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ikishuhudiwa na mashabiki lukuki wa muziki wa Taarab huku mtandao wako wa FULLSHANGWE ukiwa ni mmoja wa mashuhuda. Uzinduzi huo ulioambatana na Jahazi Molden Taarab kutimiza miaka 5 ilidhaminiwa na kinywaji cha Serengeti Lager kinachozaliswa na kampuni ya bia ya Serengeti (SBL)
Mwanamuziki Mzee Yusuf ambaye pia ni kiongozi wa kundi hilo akiingia ukumbini kwa staili ya aina yake huku akilakiwa na mashabiki wa muziki wa Taarab.
Mmoja wa kundi hilo Aisha Mahamoud akipagawisha mashabiki mbvele ya Camera na mashabiki wake.
Keki Maalum ya miaka 5 ya Jahazi Molden Taarab ikisubiri kuliwa na wapenzi wa bendi hiyo.

No comments:

Post a Comment