Pages

Pages

Saturday, December 24, 2011

KIGOGO WA CHADEMA ADAIWA KUNASWA KWA MGANGA WA KIENYEJI

MBUNGE wa viti maalum Katika moja Kati ya mikoa ya nyada za juu kusini kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) jina na mkoa wake vinahifadhiwa, amenaswa akiwa kwa mganga wa kienyeji (Sagoma) akifukizwa dawa pamoja na gari lake majira ya jioni katika eneo la Ilala mjini Iringa.
Reporter wa Mtandao wa www.sufianimafoto, kutoka mkoani Iringa anaripoti kuwa mbunge huyo alionekana akiwa kwa Sangoma huyo baada ya vyanzo vyetu vya habari kubonyeza juu ya tukio hilo .
Japo haikufahamika ni ugonjwa gani mbunge huyo alikuwa akitibiwa ila bado mtandao huu na mashuhuda wa tukio hilo walipata kushuhudua gari la mheshimiwa huyo likizindikwa (kuimarishwa) zaidi kwa dawa na Sangoma .
Baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa wabunge mbali mbali wamekuwa wakifika eneo hilo kupata zindiko kutoka kwa Sangoma huyo ambaye amekuwa akipuuzwa na wenyeji wa eneo hilo huku wageni wakihangaika kumtafuta hasa waheshimiwa.

No comments:

Post a Comment