Pages

Pages

Saturday, December 24, 2011

MISS UTALII DUNIA KUFANYIKA TENA TANZANIA 2012

Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa shindano la kumsaka Miss Utalii wa Dunia mwaka 2006 mara walipomtembelea IKULU (Picha na Maktaba ya Miss Utalii ORG.
Rais Kikwete akiwa na Gideon Chipungahelo (Chips)
Tanzania kwa mara nyingine tena imepewa heshima ya kuwa wenyeji wa fainali za Dunia za Miss Utalii ,ambapo safari hii , Kamati ya Dunia ya Miss Tourism United Nation Organisation, imeipa heshima ya kuwa wenyeji wa shindano la Miss tourism United Nations World 2012.
Kupitia kampuni ya Miss Tourism Tanzania Organization, waandaaji wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania, Tanzania imezishinda nchi nyingine nne zilizo kuwa zikiwania fulsa hiyo adimu, nchi hizo ni pamoja na Jamaica, Korea,China,Kenya na Nigeria.
Sambamba na uteuzi huo, kamati hiyo ya Dunia imemteua Gideon E.G.chipungahelo kuwa mkurugenzi wa mashindano hayo barani afrika , na makamu wa rais wa mashindano hayo Duniani .kuanzia Novemba 1,2011.
Mashindano hayo yatashirikisha jumla ya nchi 120, duniani, na kurushwa LIVE katika TV za nchi zaidi 100 duniani kote. Pamoja na washiri hao,waandishi wa habari kutoka nchi zaidi 70 , vipngozi zaidi 120 na wanafamilia zaidi 200 wanatarajiwa kuja nchini sambamba na washiriki wa mashindano hayo. Tuna mshukuru mungu kwa kuweza kushinda nafasi na heshima hii kwa nchi yetu, hasa katika wakati huu ambapo ushindani katika sekta ya utalii na uwekezaji baina ya nchi na hata baina ya mabara ni mkubwa. Tunajisikia ufahari kwa nchi yetu na kuwa sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika kutangaza utalii,utamaduni na mianya ya uwekezaji wa Tanzania kitaifa na kimataifa. Shindano hili litatyoa fulsa ya pekee kwa Tanzania ,kutangaza utalii,utamaduni na mianya ya uwekezaji kimataifa na hata kitaifa,pia kuuthibitishia ulimwengu kuwa vivutio vikuu vya utalii Afrika ikiwemo Mlima Kilimanjaro,Ngorongoro Creators na Serengeti vipo Tanzania. Hii ni fulsa pia kwa viwanda na bidhaa za Tanzania kujitangaza kimataifa na kuingia katika masoko ya kimataifa.
Taratibu zote za mikataba za kimataifa zimekamilika,tunatarajia kutangaza rasmi tarehe ya kufanyika kwa shindano hilo nchi, wakati wa fainali za Miss Utalii Vyuo Vikuu 2011/12 – Kanda ya kati, litakalo fanyika Ijumaa , tarehe 30-12-2011 katika ukumbi wa Club la Azziz Dodoma. Shindano hilo linashirikisha zaidi ya warembo 15 kutika vyuo vikuu vilivyopo katika mikoa ya kanda ya kati, ikiwemo mikoa ya Dodoma, Singida na Tabora.
Tayari taratibu za kitaifa zimanza kufanywa ,zikiwemo za kushirikisha wadau na mamlaka mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Hatua zote madhubuti zimechukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa kwa kuzingatie uzoefu na mapungufu ya liyo jitokeza katika fainali za Dunia zilizofanyika nchini mwaka 2006,pale Ubungo Plaza 11-3-2006.
Mkataba wa kufanyika kwa fainali hizo za Dunia ,nchini umesainiwa na Rais wa Miss Tourism United Nation Organisation, Ngugu Leon Willians na Rais wa Miss Tourism Tanzania Organisation ,Gideon Chipungahelo tarehe 8-12-2011.

No comments:

Post a Comment