Pages

Pages

Tuesday, January 10, 2012

CHARLZ BABA KUFICHULIWA RASMI IJUMAA

ONYESHO maalum la kumtambulisha mwanamuziki aliyejiengua katika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta, Charles Gabriel ‘Charlz Baba’ anatarajiwa kutambulishwa rasmi katika onyesho litakalofanyika keshokutwa katika ukumbi wa Victoria Park uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam huku bendi za Mapacha Watatu, Mashujaa na Extra Bongo zikitarajiwa kusindikiza.
Mratibu wa onyesho hilo King Dodoo alisema kwamba onyesho hilo litafichua ni wapi msanii huyo atakuwa akifanya kazi mara baada ya kujitoka katika bendi yake ya zamani.
“Zamani kulikuwa na mapacha wanne lakini watatu tunawasikia katika kundi la Mapacha watatu, sasa huyu wan ne hatujui alipojificha, hivyo basi tumeandaa onyesho rasmi la kumzindua pacha wa nne na ni matumaini yangu kila kitu kitajulikana siku hiyo.

No comments:

Post a Comment