Pages

Pages

Thursday, January 26, 2012

ETI SHILOLE ACHUMBIWA NA PEDESHEE LA MAFUTA..!!

Msanii wa filamu za bongo, Zena Muhamed ‘Shilole, amesema anajisikia ni mtu mwenye furaha kwani amechumbiwa na mwanaume mmoja ambaye ni mfanyabiasha wa mafuta kutoka mkoani Tanga.

Msanii huyu kwa muda mrefu amekuwa akitafuta mwanaume wa kumuoa ambapo sasa anaonekana kuwa na furaha kwani ndoto yake ya imetimia.

Shilole alisema kuwa ndoa yake itafungwa muda wowote baada ya maandalizi yote kukamilika ambapo inaweza kufungwa mwezi Octoba mwaka huu. Hata hivyo aliongeza kuwa ndoa hiyo itafungwa kimila na si kama watu walivyozoea kufunga zile za kifahari.

“Yani naweza kusema kuwa mwaka huu utakuwa wa furaha sana katika maisha yangu, kwani nimepata mwanaume ambaye ndiye chaguo langu na kikubwa ni kwamba ndoa yetu tutafunga kimila,” alisema.

Msanii huyu yupo mkoani Tanga ambapo ameenda kwa lengo la kujiachia kidogo na mchumba wake huyo ambaye hakutaka kumtaja jina.

No comments:

Post a Comment