Pages

Pages

Thursday, January 19, 2012

JINI KABULA NA JACK WA CHUZI WAGOMBEA PENZI LA CHUZI

WASANII wawili wa bongo movie Jack wa Chuz na Jini Kabula, wameingia katika mzozo kwa kile kilichodaiwa kuwa wameanza kujirudi kwa aliyekuwa mpenzi wao wa zamani Mr Chuzi huku wakipeana vijembe vya chinichini.

Sakata hilo limetokea hivi karibu ndani ya viwanja vya Leaders Club, ambapo wasanii hao walikuwa wakipata vinywaji na baada ya muda mfupi walionekana kuzozana huku wakitaja jina la mpenzi wao huyo.

Wakati nyota hao wakiendelea na mzozo huo, mwandishi wa habari hii alifika eneo hilo na kukuta hali ya hewa ikiwa siyo nzuri huku baadhi ya marafiki zao wakiwa nyuma.

Piailizungumza na baadhi ya watu walioshudia mzozo huo ambapo walisema kuwa awali wasanii hao walikuja hapo wakiwa na furaha lakini baada ya kunywa walianza kumtaja mpenzi wao huyo kutokana na mambo aliyowahi kuwafanyia.

“Unajua awali walikuwa wakizungumza kawaida lakini baada ya vinywaji walivyokuwa wanakuywa kuwakolea wakaanza kumtaja Chuzi tena kwa sauti kubwa, na sisi hatukujua kama watafikia hatua ya kushikana na kufanya hali ya hewa kuchafuka,” alisema mmoja wa shuhuda aliyeshudia mzozo huo ambaye hakutaka jina lake liandikwe.

Hata hivyo  baada ya kuona wasanii hao wametulia likaamua kuzungumza nao ambapo wote walikiri kuwa wanataka kuendelea na Chuzi, lakini wanashindwa kuelewana kwani wao ni marafiki.

Jini kabula alisema kuwa yeye anampenda Chuzi, kwani ni mtu ambaye alimsaidia kumtoa hadi kufika hapo alipo lakini anashindwa kuvumilia pale anapozushiwa maneno kuwa anataka kujirudi ili aendelee kuwa na Chuzi.

“Hakuna kitu chochote hapa lakini Jack mara nyingi amekuwa akitoa maneno kuwa mimi nataka kujirudi kwa Chuzi wakati hamna kitu kama hicho ingawa nampenda sana,” alisema.

Naye Jack alipoulizwa na Mwandishi wa habari hii, kama anahitaji kujirudi kwa mpenzi huyo wa zamani alijibu kuwa hapana ingawa mara nyingi amekuwa akizungumza naye kuhusu jambo hilo ambalo linaonekana gumu kwa upande wa Chuzi.

No comments:

Post a Comment