Pages

Pages

Friday, January 20, 2012

MAANDAMANO YA AMANI YA WANAFUNZI WAKIISLAMU SHULE YA SEKONDARI NDANDA

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akizungumza na wanafunzi waislamu waliofanya maandamano ya amani katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam leo kupinga Uongozi wa Shule ya Sekondari Ndanda kuwafukuza wanafunzi 20 wa kiislamu waliokuwa wakisoma katika shule hiyo.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa akiwasili katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam leo kuzungumza na wanafunzi wa kiislam waliokuwa wameandamana leo kupinga Uongozi wa Shule ya Sekondari Ndanda kuwafukuza wanafunzi 20 wa kiislamu waliokuwa wakisoma katika shule hiyo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Suleima Kova akiagana na  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru Kawambwa.
Rais wa Wanafunzi wa kiislamui, Jafari Mneto akizungumza katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es salaam baada ya Wanafunzi wa Kiislamu kufanya maandamano.
Wanafunzi wa kiislamui Shule ya Sekondari Ndanda wakiwa katika viwanja vya Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment