Pages

Pages

Saturday, January 14, 2012

MBUNGE WA CHADEMA REGIA MTEMA AFARIKI DUNIA

Mbunge wa viti Maalum Chadema kutoka Kilombero mkoani Morogoro, Regia Estelatus Mtema amefariki dunia hii leo kwa ajali ya gari.
Taarifa iliyoifikia Blog ya hii ya Jamii hivi punde toka Ruvu Mkoano Pwani, zimesema kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),amefariki katika ajali mbaya ya gari mapema leo asubuhi katika eneo la Ruvu  wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Morogoro. 
Kwa Mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa mbunge huyo ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe gari lake amepinduka na gari hilo mara baada ya kumshinda wakati akijaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake katika eneo hilo la Ruvu.
Ndani ya Gari hilo kulikuwa kuna watu wengine wanne ambao bado hawajatambulika ni kina nani na wako kwenye hospitali ya Tumbi Kibaha mkoani Pwani kwa Matibabu.
tutaendelea kujuzana zaidi kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.

No comments:

Post a Comment