Pages

Pages

Wednesday, January 11, 2012

MENEJA WA TIPTOP NA TUHUMA ZA UCHAWI

 Meneja wa kundi la TIPTOP CONNECTIONS Babtale  leo amezungumzia tuhuma zilizoenea kuhusu yeye kwamba ni MCHAWI, stori ambazo zimeandikwa na mitandao mbalimbali.
 

 Moja kati ya mitandao hiyo, umeamplfy kwamba boss huyo wa Tip top connection ni mchawi na huwa anatembea na kibegi chake flani, hakiachi hata awe anaenda, ambapo ukichunguza utagundua kwamba msanii yoyote atakayeingia tiptop connection alaf akaondoka baadae, ndo unakuwa mwisho wa career yake, yaaani lazima apotee kwenye muziki hata kama atajitahidi vipi, mfano ni kwa MB DOGG, PNC, Z ANTO, PINGU, KEISHA na sasa KASSIM ambae ameondoka juzijuzi lakini bado anasikika kiaina ila inasemekana muda c mrefu atachuja.

 hichi ndio kibegi cha Babtale, kinachotajwa kuwa na uchawi wake!
kwa kujibu, Babtale amesema “kuna mambo mengi nafanya mazuri lakini watu hawayaoni, kibegi changu nakitumia kuhifadhi vitu vyangu, kuna laptop na vitu vingine ninavyohifadhi, mtu anaponiandika kwamba Tale mchawi amempoteza msanii huyu, amemdidimiza msanii huyu, wnaashindwa kuelewa kwamba mwanzo mimi ndio nilifanya huyo msanii anga’e, na akiondoka kuwa chini yangu wengi wanafeli kwa sababu hawana MANAGEMENT nzuri”

   Babtale anaeongoza TIPTOP CONNECTION iliyotimiza miaka 10 mwishoni mwa mwaka jana, ameongeza kwamba “kuna mambo mengi nafanya lakini hakuna anaesifia, mimi na Said Fela wa TMK family ndio tunamsimamia DIAMOND sasa hivi, tumemrudisha Ferooz na mchiriku wake, tumemrudisha SUMALEE lakini hakuna anae tusifia, watanzania hawakusifii mpaka Ufe, sio kitu kizuri” – BabTale 

No comments:

Post a Comment