Pages

Pages

Saturday, January 14, 2012

MKUU WA MKOA WA RUKWA AZINDUA KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA MJINI SUMBAWANGA.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akifagia kwenye moja ya barabara za Mji wa Sumbawanga Mkoani humo jana katika uzinduzi wa kampeni ya kusafisha Mji huo ijulikanayo kama "SUMBAWANGA NG'ARA 2012". Wanaojumuika naye kwenye usafi huo ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga Samwel Simwela. Mkuu huyo wa Mkoa ameanzisha Kampeni hiyo ambayo itakuwa ni ya kudumu baada ya kuona Manispaa hiyo imezorota katika usafi wa mazingira
Wananchi wa Manispaa ya Sumbawanga walihamasika na kumuunga mkono Mkuu wa Mkoa wa Rukwa katika kampeni hiyo.
Huku Mkuu wa Mkoa huo akiendelea na ufagiaji wa barabara za Mji huo wa Sumbawanga Daladala nazo zilikuwa zikiendelea na shughuli zake za kusafirisha abiria kupitia barabara hizo. Nyuma yake ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao.
Waandishi wa habari nao walikuwepo kutaka kujua kilichomsukuma Mkuu wa Mkoa huo kuamua kuingia barabarani na kuanza kufagia, ambapo alisema Kiongozi bora ni lazma afanye kazi kwa vitendo na kuwa mfano bora kwa wale anaowaongoza.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa mchanga kwenye mtaro katika moja ya barabara zilizopo katikati ya Manispaa hiyo ya Sumbawanga huku Mvua ikiendelea kunyesha.
Mbunge wa jimbo la Sumbawanga Mjini Mhe. Aeshi Hillal akitoa uchafu kwenye mtaro katika moja ya barabara zilizopo katikati ya Mji wa Sumbawanga wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jana. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Mohammed Chima na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Sabas Katepa

No comments:

Post a Comment