Pages

Pages

Thursday, January 19, 2012

MTOTO WA MIAKA TISA AJERUHIWA KWA MIJEREDI KAMA NG'OMBE WA KILIMO NA SHANGAZI YAKE

Picture
Mtoto mdogo wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka tisa,amelazwa wadi namba saba katika Hosiptal ya Mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi akiuguza majeraha aliyoyapata yanayodaiwa kutokana na kipigo ambacho amekuwa akikipata kutoka kwa shangazi yake ambaye ni Mwalimu wa shule ya Msingi Narumu iliyopo wilaya ya Hai.  Mtoto huyo ambaye kwa sasa ameathirika kisaikolojia kutokana na tukio hilo,inadaiwa na wasamalia wema kuwa,mwanamke huyo amekuwa akimpa vipigo mara kwa mara kwa kutumia waya.  Taarifa ya jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro iliyotolewa kwa vyombo bya habari imedhibitisha ukatili dhidi ya mtoto huyo na kwamba mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Anna John(28)mkazi wa mtaa wa  Kiusa katika Manispaa ya Moshi, bado anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.  Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ni matokeo ya wanawake wanaojihusisha na uuzaji wa mboga mboga na matunda  wa mtaa wa Kiusa mjini Moshi kuamua kufuatilia nyendo za mtoto huyo baada ya kutumwa sokoni na mtuhumiwa na kisha kurejea tena sokoni akiwa analia na kuwapa hofu kina mama waliokuwa sokoni na kuhoji kulikoni.

No comments:

Post a Comment