Pages

Pages

Thursday, January 12, 2012

SHEREHE ZA MIAKA `48 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Kikosi cha Wanajeshi waenda kwa miguu, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu na kutoa heshima kwa mgeni wa rasmi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Moahmed Shein akizungumza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete,katika kilele cha Sherehe za miaka 48 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar,zilizofanyika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo.
Kikosi cha kutuliza ghasia FFU, kikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa haraka na kutoa heshima kwa Mgeni rasmi. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Abeid Karume, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar leo Januari 12, kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 48 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Moahmed Shein akimakaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete,katika kilele cha Sherehe za miaka48 ya mapinduzi matukufu ya zanzibar,zilizofanyika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Kutoka kulia Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Benjamin Mkapa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk Aman Abeid Karume na Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar Mh Ramadhani Haji Fakhi
Katikati ni Makamu wa Kwanza wa Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad kulia Mkewa wa Rais Mama Salma Kikwete na kushoto ni Mke wa makamu wa rais Mama Asha Bilal wakiwa katika sherehe hizo. 
Vijana wakipita mbele ya Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi wengene wa Serikali pamoja na mabalozi huku wakiwa wameshika picha ya Mzee Abeid Amaan Karume Mwaasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa sherehe hizo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Moahmed Shein akikagua gwaride katika maadhimisho hayo leo mjini Zanzibar.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria katika sherehe hizo wakishuhudia shamrashamra za maadhimisho hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Moahmed Shein akiwasili kwenye uwanja wa Amaan tayari kuongoza sherehe za miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar. 
Wananchi wakishuhudia sherehe hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa Amaan mjini Zanzibar leo. (Picha na Ikulu).

No comments:

Post a Comment