Pages

Pages

Wednesday, January 18, 2012

SHILOLE ANADAIWA KODI SH. MIL 6, APEWA MWEZI MMOJA WA KULIPA

MSANII nyota wa filamu Zena Muhamed ‘Shilole’, yupo katika wakati mgumu kimaisha kwani anadaiwa zaidi ya sh, Milioni 6, kama kodi ya nyumba anayoishi huku akiwa na madeni kwa baadhi ya majirani zake ambapo amepewa muda wa mwezi mmoja awe amelipa pesa hizo.

Msanii huyu anaishi nyumba ya kupanga maeneo ya kinondoni, na inadaiwa kuwa hakulipa kodi kwa muda mrefu kwa kile kinachodaiwa kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia nyumbani kwao Arusha ndiyo maana hakuweza kulipa kodi hiyo.

Akizungumza Jijini Dar, ili kueleza ukweli wa habari hizo Shilole, alisema ni kweli anadaiwa lakini yupo katika mchakato wa kulipa pesa hizo kwani kwa muda mrefu alikuwa akituma pesa nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu ya ndugu zake.

Alisema kuwa tangu June mwaka jana hakulipa kiasi cha pesa alichokua akidaiwa hivyo mama mwenye nyumba amempa muda wa mwezi mmoja awe ametoa pesa hizo.

“Jamani ni kweli nadaiwa pesa hizo, lakini nilishindwa kulipa kwani ndugu zangu walikuwa wanaumwa hivyo pesa zote nilizitumia kwa ajili ya matibabu,” alisema.

Hata hivyo aliongeza kuwa baadhi ya majirani zake wanamdai zaidi ya shs laki 7, ambapo hajui atazitoa wapi kipindi hiki ambacho yupo kwenye matatizo kama hayo.

No comments:

Post a Comment