Pages

Pages

Thursday, January 5, 2012

SIMBA YANYOLEWA SHARUBU NA WAPEMBA


MSHINDI wa pili wa ligi kuu ya Zanzibar timu ya Jamhuri yenye mastakimu yake mtaa wa chasasa kisiwani Pemba jana waliianza vyema michuano ya mapinduzi Cup baada ya kuifunga timu ya Simba ya Dar es salaam mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wawanja Amani mjini Zanzibar
Mechi hiyo kati ya Simba na Jamhuri ambayo ilichezeshwa na mwamuzi Juma Ali ilikuwa ya kuvutia na ya kupendeza hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu ambayo ililiona lango la mwenzake japo kuwa juhudi za kufunga zilikuwa zimefanyika kwa timu zote lakini kwa bahati mbaya hakuna timu ilifunga kipindi hicho cha kwanza.
Katika mechi hiyo ambayo ilihudhuriwa na wapenzi wengi wa soka wa Zanzibar ilikuwa ni timu ya Jamhuri ambayo ilipata bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji Ali Othman Mmanga katika dakika ya 10 ya kipindi cha pili cha mchezo huo
Kama hiyo haitoshi timu ya Jamhuri ambayo ilikuwa ikicheza kwa uwelewano mkubwa iliandika bao la pili katika dakika ya 21 bao hilo lilifungwa na Ali Bakar na kumuacha mlinda mlango wa Simba Ali Mustafa Batezi akiwa hana la kufanya
Timu ya Simba itashiriki katika michuano ya kombe la shirikisho na ambayo ilikuwa imechezesha wachezaji mchanganyiko wale wa zamani na damu changa kutokana na uzoefu wao kabla ya kumalizika kwa pambano hilo walipata bao la kufutia machozi bao ambalo lilifungwa na beki wao anayepanda na kushuka Shomari Kapombe
Kocha wa timu hiyo ya Simba alipoulizwa juu ya pambano hilo kwanini amepoteza mchezo huo alisema kuwa mabeki wa timu, hiyo walifanya makosa ambapo wenzao wa timu ya Jamhuri wameyatumia na kushuinda mchezo huo
Kabla ya kufungwa kwa timu ya simba hapo jana mabao 2-1 katika mfululizo wa michuano ya kombe la Mapinduzi Cup, timu ya Yanga nayo ya Dar es salaam tayari imekwisha fungwa bao 1-0 na timu ya Mafunzo ya Zanzibar
Katika kinyanganyiro hiki cha michuano ya kombe la Mapinduzi kutimia miaka 48 timu zinazoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na timu ya Jamhuri, Mafunzo, Kikwajuni, Yanga, Simba, na timu ya Azam FC wanaramba ramba
Aidha katika mashindano hayo ya mapinduzi Cup kutimiza miaka 48 ya mapinduzi ya Zanzibar pia zipo timu za kikosi maalumu cha kuzuia magendo KMKM pamoja na Miembeni United.

No comments:

Post a Comment