Pages

Pages

Tuesday, January 24, 2012

TANI 40 ZA DAGAA ZAKAMATWA ZIKISAFIRISHWA KWA NJIA YA MAGENDO KUELEKEA NCHINI KENYA

Gari aina ya roli mali ya Grace Enterprises ya Nairobi nchini Kenya yenye namba za usajili KBJ 409 W na tela lake lenye namba za usajili ZC 9486 limekamatwa likisafirisha kwa magendo mzigo wa dagaa unaokadiriwa kuwa na uzito wa zaidi ya tani 40 ukitoka katika bohari ya kuhifadhia kijiji cha Nyamikoma wilayani Magu mkoani Mwanza njiani kuelekea nchini Kenya kwaajili ya biashara.
Afisa wa polisi akichukuwa maelezo toka kwa mmiliki wa roli hilo Godfrey Mwangi mara baada ya dereva kulitelekeza gari hilo na kutoweka kusiko julikana.

No comments:

Post a Comment