Pages

Pages

Friday, January 6, 2012

THIERRY HENRY ARUDI EMIRATES


Thierry Henry amekamilisha uhamisho wa muda mfupi kurudi Arsenal.
The Gunners wamekamilisha makubaliano ya bima na New York Red Bulls, kwa maana Henry sasa anaweza kuanza kuichezea Arsenal kuanzia Jumatatu katika raundi ya Kombe la FA dhidi ya Leeds.
The 34-year amesajiliwa kama mbadala wa Gervinho na Maroune Chamakh, ambao watakuwa wakielekea Africa kucheza CAN na timu zao za taifa Morocco na Ivory Coast.
Henry alisema: “Ni vigumu kuwa mkweli lakini linapokuja suala la Arsenal moyo ndio utakaokuwa unaongea.
“Tangu nilipojua the plan nyuma ya usajili wangu nilikuwa sawa na kurudi Gunners. Sijarudi Arsenal ili kuwa shujaa au ku-prove kitu chochote. Nimerudi kusaidia tu.
“Watu wanabidi waelewe kwamba Chamakh na Gervinho wanaenda kucheza CAN, hivyo niliitwa kuja kujaza gap waliyoiacha.”
Henry atavaa jezi namba 12 mpaka atakapomaliza mkataba wake wa miezi miwili.
Welcome The Greatest King Theirry Henry.

No comments:

Post a Comment