Pages

Pages

Thursday, January 26, 2012

ZIARA YA WAZIRI WA BIASHARA KUTOKA SWEDEN DKT. EWA BJȌRLING NCHINI TANZANIA

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (Mb) akizungumza na ujumbe kutoka Sweden uliomtembelea kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini mapema mchana leo. Ujumbe huo uliongozwa na Waziri wa Biashara wa Sweden Dkt. Ewa Bjȍrling na Balozi wa Sweden – Tanzania, Bw. Lennarth Hjelmaker. Nia ya ujumbe huo ni kuangalia fursa za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo.
Balozi wa Sweden Nchini Bw. Lennarth Hjelmaker akisisitiza jambo mara ujumbe wa Sweden ulipofanya kikao na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (Mb.) kwenye ofisi za Wizara mapema leo mchana.
Waziri wa Biashara Sweden Dkt. Ewa Bjȍrling akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini zawadi mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha ujumbe kutoka Sweden na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Nia ya ziara ya ujumbe huo ni kubaini fursa za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo.

No comments:

Post a Comment