HUDUMA ZA KLINIKI ZASITISHWA MUHIMBILI
MGOMO
wa madaktari umezidi kutikisa na kuathiri huduma za afya katika
hospitali kuu nchini, huku Taasisi ya Mifupa (Moi) ikitangaza rasmi
kufunga kliniki zote zinazohudumia wagonjwa wa nje hadi mgomo huo
utakapomalizika.Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Profesa Lawrence Museru
alitangaza uamuzi huo wa kufunga huduma hizo jana, akisema taasisi hiyo
ina madaktari bingwa 30 pekee na ndiyo wanaofanya kazi huku madaktari
wake wengine zaidi ya 30 wakiwa kwenye mgomo. Alisema
kufuatia hatua hiyo, madaktari waliobaki hawawezi kujigawa na kuhudumia
wagonjwa wote wanaofika katika taasisi hiyo na ndiyo sababu,
wamelazimika kusitisha huduma kwa kliniki.
No comments:
Post a Comment